Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morrice Oyuke (kushoto), akizungumza katika mkutano na wanahabari Dar es Salam leo asubuhi kuhusu pato la Taifa kwa robo ya pili ya mwaka kuanzia Aprili hadi Juni-2014. Kulia ni Mtakwimu Mwandamizi, Jovita Rugemalira na Mtakwimu Mkuu Uchumi, Adela Ndesangia.
Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morrice Oyuke (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Mtakwimu Mkuu Uchumi, Fred Matola. Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Dotto Mwaibale
SEKTA ya kilimo na uvuvi imeongeza pato la taifa kwa asilimia 5.4 ukilinganisha na asilimia 4.9 kwa mwaka 2014.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morrice Oyuke Dar es Salaam jana wakati akizungumza katika mkutano na wanahabari kuhusu pato la taifa kwa robo ya pili ya mwaka kuanzia Aprili hadi Juni-2014.
Alisema katika kipindi hicho shughuli za kilimo na mazao zilikuwa kwa asilimia 6.5 mwaka huu ukilinganisha na asilimia 5.3 mwaka 2013 na kuwa shughuli za mifugo zilikuwa kwa
asilimia 0.9 mwaka 2014 ikilinganishwa na asilimia 3.8.Oyuke alisema shughuli za misitu na uwindaji zilikua kwa asilimia 0.8 mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 3.2 kwa
mwaka 2013.
Alisema katika Sekta ya viwanda na ujenzi shughuli za uchimbaji madini, mawe na kokoto ziliongezeka na kufikia kasi ya asilimia 3.0 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka huu ilikilinganishwa na kasi ya ukuaji wa asilimia hasi 6.2 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2013.
Oyuke alisema kuongezeka kwa kasi hiyo kulitokana na uzalishaji wa madini ya almasi na Tanzanite katika robo ya pili ya mwaka huu.Hata hivyo Ayuke alisema uzalishaji wa dhahabu ulipungua katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2014.