Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
UEFA, kufuatia fujo za mashabiki zilizojitokeza wakati wa mchezo wa kundi la nne uliozikutanisha klabu hizo usiku wa kuamkia jana jijini London.
Taarifa iliyotolewa na UEFA imedai kwamba, utaratibu wa kuchunguza utovu huo wa nidhamu bado unaendelea, na Arsenal wanaingia katika mkumbo wa kuadhibiwa na shirikisho hilo kutokana na kushindwa kuweka mikakati madhubuti ya kuwazuia mashabiki wa Galatasaray kuingia na mafataki uwanjani.
FC Basel nao watakumbana na adhabu kutoka UEFA, baada ya mashabiki wao kutupa fataki uwanjani wakati wa mchezo wa kundi la pili dhili ya Liverpool, uliochezwa usiku wa kuamkia jana na wenyeji kuibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa mabingwa hao wa Uswiz kuadhibiwa na UEFA, baada ya kukumbana na adhabu ya kucheza katika kiwanja huru msimu uliopita wakati wa mchezo wa hatua ya robo fainali wa michuano ya Europa League.
Borussia Dortmund nao wanatuhumiwa na UEFA kwa utovu wa nidhamu ulioonuyeshwa na mashabiki wao wakati wa mchezo wa kundi la nne dhidi ya Anderlecht waliokubali kufungwa mabao matatu kwa sifuri.
Katika mchezo huo mashabiki kutoka nchini Ujerumani walionekana, wakihama kutoka sehemu moja kwenda nyingine huku wakiwa wameshika mafataki mikononi, hali ambayo imetafsiriwa kama kitendo cha kuthubitu kuvunja amani