Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Muigizaji wa filamu nchini Nisha Salma Jabu juzi aliwaacha watu hoi wakati wa utoaji wa tuzo za Action And Cut Viewers Choice Awards zilizofanyika Sunrise Kigamboni.
Baada ya kutajwa jina lake kuwa ndiye mshindi wa mchekeshaji bora wa kike(Best comedienne) Nisha alionekana kupagawa kwa furaha ya kutoamini huku baadhi ya watu wakimshangaa star huyo kwa furaha aliyokuwa nayo. Hata hivyo Nisha aliweka wazi kuwa hakuamini kama kuna siku atakuja kupata tuzo kutokana na kazi zake za filamu ambapo amesema anajitahidi kufanya akazi bora kila siku.