Bomu ambalo liliokotwa na mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Mji Mpya Emmanuel Stanley jirani na kambi hiyo ya zamni ya wakimbi wa Afrika kusini..
Mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya Sekondari ya Kata ya Mji Mpya Emmanuel Stanley (17) ameokota bomu viwanja vya kanisa maombi na maombezi lililopo eneo la Barakuda Kata ya Mazimbu manispaa ya Morogoro jirani na iliyokuwa kambi ya wakimbizi wa Afrika Kusini.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Bila kujua kama hilo ni bomu mwanafunzi huyo alianza kulicheza kabla ya mwenzake aliyefahamika kwa jina moja la Evon kumshtua kwamba hilo ni bomu ambapo kwa pamoja wanafunzi hao walitoa taarifa kwa wazazi wao ambao nao walitoa taaria kwa serikali ya mtaa huo
Geti kuu la kuingia campus ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine[SUA] ambayo zamani ilikuwa kambi ya Wapigania uhuru wa Afrika Kusini
CHANZO : MATUKIO BLOG
Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa Bw Kaloli Joseph Poul akimuoneysha bomu hilo
Akihojiwa na mwandishi wetu mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Modeko 'B' Bw Kaloli Joseph Poul amethibitisha kuwepo kwa bomu hilo katika mtaa wake na kudai.
" Nikweli kama unavyoliona bomu hili limeokotwa na mwanafunzi Emmanuel kwenye eneo hili la kanisa,awari mwanafunzi huyo hakugundua kama ni bomu ambapo alilichezea kwa muda kabla ya mwenzake aliyefahamika kwa jina moja la Evon kumstua kwamba hilo ni bomu kwa pamoja watoto hao walitoa taarifa kwa wazazi ambao nao walitujulisha sisi viongozi wa mtaa na kwamba nasisi tuli ripoti tukio hilo Polisi"alisema mwenyekiti huyo na kuendela kusema.
"Kundi la mapolisi 12 waliojaa kwenye Difenda mbili walifika eneo hilo na tukio na kuthibitisha kwamba hilo ni bomu ambapo nao waliwaita wanajeshi wa kikosi cha Mzinga ambao baada ya kufika walidaikwamba bomu hilo ni la muda mrefu na kwamba linaweza kulipuka wakati wowote hivyo kwa muda huu wamekwenda kambini kwao kuchukua vifaa kwa lengo la kuja kulilipua hapa hapa na kwamba wamedai kwamba wakati shughuri hiyo ya kulipua bomu hilo ikifanyika wananchi wote wanatakiwa kuondoka katika mtaa huu umbali wa mita 400 na sisi kama viongozi wa mtaa tayari tumeshawatangazi wananachi wetu na kwamba kwa sasa eneo hili lina lindwa na polisi"alisema kiongozi huyo wa mtaa
Kwa upande wake mchungaji wa kanisa hilo Bi,Tabia Mwalusako alipohojiwa na mwandishi wetu alisema anamshukuru Mungu kwa kuendelea kuwalita na tukio hilo la hatari
" Tukio hili limetustua sana lakini mungu wetu ambaye ni Mlinzi wa maisha yetu ametulinda hebu fikiria watoto wale waliliokota bomu lile na kulichezea kwa dakika kadhaa bila kuwazulu pia nitumia fursa hii kukanusha habari zilizozagaa mjini kwamba tukio hili linahusihwa na ugaidi wazee wa eneo hili walisema kwamba campus hii ya SUA awari ilikuwa akikaliwa na wakimbi wa Afrika kusini hivyo bomu kuonekana eneo hili sio jabo la ajabu zaidi ya yote bomu hili lilifukiwa muda mrefu ardhin kabla ya kuokotwa na hawa watoto waliokuwa wakilima kwenye bustan hii"alisema Mchungaji huyo.