Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Wewe kama ni mwanamke ambaye umeolewa na mme wako amekuwa akibadilisha kazi au kufanya kazi sehemu tofauti tofauti na miji tofauti tofauti basi atambue kuwa kuna kazi au biashara ambazo utafanya bila kuacha kazi au biashara hiyo. Ni kazi zinazosafiri na wewe kila utakapokwenda, huhitaji kuwa sehemu moja ili kazi ifanyike unahitaji vitendea kazi tu.
1. Wakala wa mauzo ya Madawa
Wakala wa mauzo yeyote anaweza kufanya kazi hiyo popote katika mji wowote nchini, kwani kila mji una hospitali na maduka ya madawa hivyo una wateja kote nchini.Na Kazi hizi zinahitaji watu waliosomea taaluma hiyo inayohusiana na madawa ya binadamu.
2. Wakala wa mauzo ya Bima Mbalimbali
Wakala wa Mauzo ya bima anasaidia watu wapate bima zao pale wanapohitaji, hivyo kama makampuni ya bima yana ofisi nchi nzima au mawakala nchi nzima hivyo unaweza kufanya kazi hii popote pale utakapokwenda na ukapaka kamisheni ya mauzo ya bima hizo. Kazi hizi zinawafaa watu ambao ni waaminifu na ni rahisi kutengeneza urafiki.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
3. Mwalimu wa Kiingereza na Hesabu
Kila sehemu tumekuwa na tatizo la walimu wa Kiingereza na Hesabu , hivyo wewe kama ni mwalimu mzuri kila utakakokwenda utapata kazi. Unaweza kuanzisha masomo kwa wanafunzi baada ya muda wa kawaida wa masomo au vinginevyo ila inahitaji ujasiri, uvumilivu na ubunifu ili use mwalimu bora na mwenye matokeo makubwa.
4. Wakala wa Malipo na Mauzo ya Huduma
Kama wakala wa mauzo ya Bima kwa sasa Tigo pesa, Mpesa, Maxmalipo zimetengeneza ajira za kutosha sehemu nyingi. Ukifikiria kwa upana zaidi kuna vitu vingi ambavyo unaweza kufanya na kuwasaidia watu mahali popote utakapokuwa.
5. Mwandishi wa Kujitengemea
Kwasababu waandishi wengi wa kujitegemea hufanya kazi kutokea nyumbani, inamaanisha wanaweza kufanya kazi kutokea mahali popote wakati wowote. Kuwepo kwa mtandao wa intaneti sehemu nyingi au nchi nzima huwezi kupoteza kazi yako ni wewe tu kujua nini unafanya.
Kama maisha yako yanabadilika badilika au umekuwa ni mtu wa kuhamahama ni vizuri kuwa na njia mbadala wa kila unachokifanya. Kuna kazi nyingi ambazo unaweza kuzifanya sehemu mbalimbali inahitaji wewe kufikiri kwa marefu na mapana. Hizo ni baadhi tu ya zile unazoweza kuzifanya na haziathiriki pale unapoamua kuhama mji au kutoka jiji moja kwenda jingine.