CEO wa MJ Records na mtayarishaji nguli wa muziki nchini, Joachim Kimaryo aka Master J anafahamika kwa kutouma maneno pale anapoamua kufunguka yaliyo ndani ya moyo wake.
Akihojiwa kwenye kipindi cha ‘The Jump Off’ cha kituo cha radio cha Times FM wiki hii, Master J aliamua kudondosha ‘bombshell’ kuwa wasanii wa Bongo ni wezi.
“Huwezi kuchukua wazo langu uende kulitumia kutengeneza hela halafu uniambie kwamba ‘bwana mimi sikupi kitu’, wasanii ni wezi tu Bongo,”alisema.
“Watu wanaogopa kuongea, mimi ngoja niongee tu ukweli, wasanii wa Bongo ni wezi. Kitu wanachokifanya ni wizi. Unajua mwizi anakaaga kimya, lakini wanakwenda kwenye media wanaropoka ‘nimeingiza milioni 300, kwa kutumikia haki ya Lamar bure na simpi kitu. Yaani unaiba halafu unaenda unatangaza kwenye media?
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
“Hata hawaogopi! Walivyokuwa hawajui kwamba sheria hairuhusu kufanya hivyo, na kiukweli akiamua kupania anapata cha kwake, sema tu maproducer hawafuatilii. Lakini wanavunja sheria kabisa na ni wezi. Huwezi kufanya hivyo halafu unaenda unatangaza, kaa kimya…kula na kipofu. Sio sawa wanavyofanya.”
Source: Timesfmwebsite