Ninafikiri watu wengi tumewahi kukutana na swali, kwanini unafanyi hivi au vile? Na hata kwenye filamu moja ya marehemu Kanumba aliigiza filamu inaitwa , Why? Hilo ni swali lile lile katika mtizamo tofauti. Ukitaka kujua uwezo wa kufikiri kwako ni pale utakapojibu kwa usahihi hili swali, kwanini?
Mfano; Kama wewe ni mfanyakazi ukaulizwa kwanini unafanya kazi? na kutokana na jibu lako ukaulizwa tena kwanini? na kutokana na jibu lililofuata ukaulizwa tena kwanini? na kutokana na jibu hili tena ukaulizwa kwanini? Kinachofuata hapo watu wengi huchanganyikiwa au hukasirika kwasababu huanza kuishiwa majibu au swali hilo huanza kuchimba undani na uhalisia wa mtu.
Nataka niongelee umuhimu wa swali hilo katika kazi, masomo au maisha yako ya kila siku. Unapaswa kujiuliza kwanini unafanya unachokifanya, kwanini uko hapo ulipo? Kwanini unafikiri hivyo ulivyo na kwanini ni wewe?
Ni eneo ambalo unaanza kuona uhalisia wa wewe na vitu unavyofanyana utagundua makosa yako mengi au mitizamo mingi ambayo sio sahihi ukihusianisha na kitu unachofanya ka kujiuliza tu kwanini?
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Hili ni moja ya mazoezi madogo sana yenye matokeo makubwa endapo utachukulia kwa uzito wa hali ya juu. Hapa tulipo ni kwasababu kwa namna moja ama nyingine tumeshindwa kujibu hilo swali na kuamua kufanya mambo kirahisi na kwa mtizamo rahisi. Unahitaji kujua ni kwanini unafanya na kuamini hicho unachokiamini na kwanini? Ili uweze kujua kama unajua kwanini upo hapo na mazingira hayo uliyonayo kwanini?
Mpaka utajikuta unapata maswali na majibu ya vitu vingi ulivyooozia kujiuliza na sasa unashangaa tatizo ni nini? Hivyo nakushauri pata ufumbuzi wa maisha yako kwa kujiuliza mara nyingi tu “kwanini?” Matokeo yake utayapata na ndipo utaanza kufanya maamuzi sahihi au yenye maelezo na sababu za kutosha.