Jeshi la polisi limeimalisha ulinzi katika maeneo yote ambayo yalitajwa na chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa ndiyo watapitia wakiandamana kwenda kwenda Bungeni kuanzia saa 4 asubuhi ya leo.(Picha na John Banda wa Pamoja Blog)
Polisi wakiwa wamefunga kamba kati barabara ya mzunguko ya stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na chuo cha biashara CBE kwaajili ya kuwazuia waandamanaji hao waliopanga kwenda Bungeni.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Polisi wapanda farasi wakiimalisha ulinzi katika viwanja vya nyerere Squere ambapo Chadema wamepanga kuanzia maandamano kuelekea bungeni.
Askali polisi wakiwafanya mawasiliano kwenye gari lao ambalo lilikuwa limepakia mbwa kwa ajili ya kuimalisha ulinzi katika viwanja vya Nyerere Dodoma kwa ajili ya kuwazuia waandamanaji wa Chadema walipanga kuandamana kwenda Bungeni.