Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

HAYA NI MAMBO MADOGO YENYE THAMANI KUBWA KWENYE MAPENZI!

$
0
0
KUNA mambo ambayo yanaweza kuonekana ya kawaida tu au si ya lazima sana lakini kumbe yana uzito na thamani kubwa sana kwenye uhusiano. Wengi wakitaka kufanya jambo la kumfurahisha mpenzi wake, huwaza katika ukubwa.

Wapo wanaofikiri labda kwa kutoka na mwezi wake kwenda naye kwenye hoteli kubwa ya kifahari ya nyota tano na kulala kwa usiku mmoja lina thamani kubwa. Pengine wapo wanaofikiri kuwa, kuwanunulia wenzi wao vitu vya thamani kubwa kama cheni ya dhahabu, gari n.k ndivyo vyenye thamani pekee!

Si kweli. Ni ukweli usio na shaka kwamba, mwanamke anapenda kufanyiwa vitu vyenye thamani na mwanaume wake. Ukweli unabaki kuwa, wakati mwingine unaweza kuwa unatamani kumfanya mwenzi wako awe na furaha muda wote lakini mfuko wako ukawa hauruhusu!

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Hulka ya wanawake wengi ni kutamani kuona mwenzi wake anamuona ni mtu muhimu na anakuwa naye karibu muda wote. Wanawake hawajali sana vitu vya thamani kama wanaume wanavyofikiri.
Kumkumbatia mwanamke na kumbusu katikati ya midomo yake, ukisindikiza na maneno matamu ni zaidi ya gari utakalomnunulia – kikubwa hapa, mwanamke huyo awe kweli ana upendo nawe na si kuwa yupo kibiashara!

Katika mada hii, nimekuandalia vitu vichache ambavyo kwa hakika, kwa mujibu wa utafiti nilioufanya, ni ‘sumu’ kwa wanawake. Ukifanya vyote au sehemu yake, unamfanya mwanamke wako ajihisi yupo katika mikono salama.
Bado thamani ya mali na vitu vingine vitabaki katika uhalisia wake, lakini kwa hakika mambo yafuatayo hapa chini, huwachanganya sana wanawake.

KADI
Ni utaratibu uliozoeleka sana kipindi cha nyuma kidogo. Sasa hivi teknolojia imeongezeka, kadi inaweza kupatikana hata kwenye mitandao mbalimbali ya internet. Hata hivyo, bado inaonekana kuwa mwanamke anapenda na anatamani kuona mwanaume wake anamkumbuka kwa kumtumia kadi.

Wanaume wengi ni wavivu, lakini kwa sababu ya ustawi wa penzi lako, jaribu hili. Nunua kadi yako yenye ujumbe mzuri, andika maneno mengine kwa mkono wako mwenyewe, pulizia manukato unayotumia, kisha mtumie/ mpelekee mpenzi wako. Utakuwa umemroga!

NYIMBO, MASHAIRI
Wanawake wanapenda sana kufahamu kuwa kweli alipo anapendwa. Nyimbo nzuri za mapenzi ambazo zitaeleza uzuri wake na namna unavyompenda na kumthamini, vinazidi kukuweka katika kilele cha umiliki uliotukuka.
Mchagulie mpenzi wako wimbo redioni, taja jina lake, lako na ujumbe wako. Utamfanya ajisikie fahari sana. Mashairi katika magazeti mbalimbali na majarida pia huongeza ladha ya mapenzi.

Anachojali mwanamke ni ile hali ya kuona kuwa, unampenda na unaweza kuthibitisha hilo hata mbele ya watu wengine. Kusikia akitajwa redioni au ameandikwa gazetini ukionyesha hisia zako za kumpenda, kutamchanganya na kumfunga kabisa hisia za kufikiri kukusaliti.

Tatizo wanaume wengi hawatilii maanani haya mambo lakini kama unataka kuwa dume la mbegu kwa mwanamke wako, jaribu uchawi huu.
Wiki ijayo itaendelea.

Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia Magazeti ya Global Publishers. Ameandika vitabu vitatu; Let’s Talk About Love, True Love na All About Love vilivyopo mitaani.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>