Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

NGOMA AFRICA BAND YAITAKIA MSONDO NGOMA BAND HERI YA MIAKA 50

$
0
0
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya, The  Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni almarufu pia kama viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens wenye makao nchi Ujerumani, inatuma salamu na saluti za kuitakia heri ya miaka 50 bendi kongwe barani afrika MSONDO NGOMA MUSIC BAND aka Baba ya Muziki ya watanzania ambayo mwezi Oktoba 2014 itatimiza miaka 50 na kuweka rekodi ya kuwa bendi kongwe pekee barani Afrika ! 

Kiongozi wa Ngoma Africa band Kamanda Ras Makunja, anaitaja bendi ya Msondo Ngoma ndiyo bendi pekee kongwe inayoendelea kutamba katima  medani ya muziki wa dansi barani Afrika na kwamba Watanzania wote duniani wana  haki ya kujivunia

Ras Makunja alisema Msondo Ngoma ilianzisha 1964 kama NUTA Jazz, baadaye ikabadili majina kama JUWATA (OTTU) kutoka na wamiliki wa mwanzo Jumuiya ya wafanyakazi Tanzania kubadili majina, na sasa ni Msondo Ngoma Band aka Baba ya Muziki, baada ya kuwa bendi inayojitegemea na siyo tena mwajiriwa wa chama cha wafanyakazi.
"Msondo Ngoma kweli ni Baba ya Muziki, maana hakuna bendi iliyo kongwe katika Afrika nzima zaidi ya Msondo", amesema Ras Makunja katika mahohiano na Globu ya Jamii kupitia mtandao wa SKYPE.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI



"Mfano bendi kongwe kama Orchestra Baobab ya Senegal ilianzishwa 1970 haiwezi kuwa kongwe! Zaiko Langa langa (DRC) ilianzishwa 1969 haiwezi kuwa kongwe mbele ya Msondo Ngoma, na T.P OK jazz ya marehem Franko wa DRC ndio ilikuwa kongwe ilianza 1956 ila sasa haipo tena

Na pia Kuna bendi ya Bana Ok Jazz  ya Simaroo Lutumba Simaroo ambayo si kongwe maana ilikuja baada ya kufa kwa Franko", anasema  Ras Makunja.
Kamanda huyomnwa FFU Ughaibuni  alisema Msondo Ngoma band ni ya Watanzania  wote na kwamba ni lazima tujivunie 

"Hongereni sana baba ya muziki Msondo Ngoma band kwa kuelekea kutimiza miaka 50. Nyinyi mmekuwa mfano wa kuigwa kwa bendi zote za muziki wa dansi Tanzania, Afrika na Dunia nzima kwa jumla. Maana pamoja na safu kubadilika kila mara kwa kuleta damu changa, lakini muziki wake ni ule ule... HONGERA SANA MSONDO NGOMA BAND, baba wa muziki Afrika!!


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>