Habari zilizotufikia hivi punde, basi la Burudani likiwa limejaza watu wengi kutoka wilayani Korogwe kuelekea Dar es Salaam, limepata ajali maeneo ya Michungwani, wilayani Handeni mkoani Tanga. Idadi kubwa ya vifo imetajwa katika basi hili. Kwa sasa watu wanatoa maiti na majeruhi wanakimbizwa hospitali ya Wilaya Korogwe, Magunga. Mwisho wa mwaka huu. Madereva kuweni makini jamani. Hali ni mbaya sana aisee. Mungu tunusuru na mabalaa ya barabarani. Picha na habari kamili zitawaijia hivi punde
CHANZO: HANDENI YETU