Kuchagua taaluma ni kufanya maamuzi ya maisha yako jinsi unavyotaka yaende. Kama yalivyo maamuzi mengine makubwa unahitaji kutumia muda wa kutosha kutafakari na kufanya maamuzi kulingana na vyanzo vya habari za kutosha kuhusu hicho unachotaka kufanya. Ingawa unaweza kusema ni mambo rahisi, kufanya maamuzi kutakana na sababu nitakazoziorodhesha ni hatari. Unahitaji kujitambua na kujiongoza vyema, vile vile unaweza kutoa ushauri wako baada ya kusoma.
Kufanya maamuzi kutakana na kile unachokiana kwenye filamu au televisheni
Nyumba si mfano mzuri wa kujua ni namna gani unaweza kufanya kazi hospitalini au ukapenda upelelezi kulingana na kile unachokiona kwenye filamu. Kama unataka kufanya taaluma fulani fuatilia kwa ukaribu maisha halisi, ongea na watu wanaofanya kazi hizo ili uweze kuja kwa marefu na mapana kabla ya kufanya maamuzi.
Kuchagua Taaluma kutokana na fedha au mshahara wake
Ndio mshahara kinaweza kikawa kigezo cha wewe kuchagua taaluma fulani lakini haipaswi kiwe kitu pekee cha kufanyia maamuzi. Fikiri zaidi ya mshahara, wewe unakuwa bora katika vitu unavyofurahia. Usipofanya kitu unachokipenda na kukifurahia kuna uwezekano mkubwa wa kuharibu kazi nakufanya vitu visivyofaa.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kuchagua Taaluma kwa sababu ya Ushawishi wa Marafiki
Kama unavyoshauliwa usichague chuo kwasababu ya marafiki hata kazi/taaluma hupaswi kufanya hivyo. hats kama unafananishwa na mtu fulani au rafiki yako wewe unavitu via tofauti na watu wengine kwenye ujuzi na taaluma.
Kuchagua Taaluma kwa sababu watu wamekuambia Utafanya Vizuri
Watu wanaweza kukusifu na kukwambia unaweza kufanya kazi fulani. Hiyo sio sababu tosha ya wewe kuchagua taaluma hiyo. Inawezekana wewe unafanya vizuri katika kuwasilisha mada au kazi za chuoni na wakufunzi wako wanasema unajua wewe utakuwa mkufunzi mzuri. Inawezekana ni wazo zuri kama ulishawahi kufikiria kuwa mkufunzi halo kabla na inawezekana hilo wazo si zuri hata kidogo kwakuwa wewe hupendi kufundisha hata kidogo. Inabidi ufikiri kwa makini kila unapopokea ushauri huo.
Kama ilivyo katika kila mambo, kuchagua taaluma sio mambo rahisi na unahitaji kuwa makini na kufikiri dana kuhusu mambo hilo. Je wewe unaushauri gani kwa watu wanaoanza kuchagua waingie kwenye Taaluma gani? Ungeweza kuwaambia nini?