Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Bibi yake Rais wa Marekani, Mh. Barack Obama, Mama Sarah Obama walipokutana leo kwenye hoteli ya Villa Rosa Kempiski jijini Nairobi, Kenya, wakati Rais Kikwete akijiandaa kurejea nchini. Mama Sarah Obama anatarajia kuzindua taasisi ya kusaidia elimu kijijini Kogelo nchini Kenya, alikozaliwa Baba yake na Rais Obama wa Marekani itakayofahamika kama (Sarah Obama foundation) ambapo atajenga shule kuanzia za awali mpaka sekondari. Rais kikwete sasa hivi yuko mjini Kondoa kuendelea na ziara yake ya Mkoa wa Dodoma. (PICHA NA IKULU)
↧