Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

UTAFITI: ZIJUE SABABU ZINAZOPELEKEA BAADHI YA WANAUME KUWA NA MPENZI WA NJE.

$
0
0


1.Kutaka kujua inauzuri gani kuwa na mwanamke mwingine nje ya huyu aliyenae. Kama ana mpenzi  mnene basi anataka tu kujua wanawake wembamba wakoje?

2.Jamii Yetu Kuhisi ni Ruksa kwa mwanaume kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja kutokana na tamaduni mbovu tulizorithi kutoka kwa mababu zetu. Mwanaume anaweza asiwe na tamaa ya kuwa na mpenzi mwingine lakini tu kwa kuona ataonekanaje kwenye jamii anaamua kuwa na mpenzi mwingine.

3. Wanaume wengi  hatujui kusema hapana; Ikitokea msichana amekushawishi basi wengi huona hili kama bahati yaani kawaacha wanaume wangapi mpaka kanifuata mimi! Kumbe unajiangamiza.

4 Marafiki wanaomzunguka; Wengi wa wanaume  hujikuta wamekuwa na wapenzi wan je kutokana tu na mrafiki anaokaa nao kuwa na tabia hii mbaya! Hivyo humbidi awe na tabia hiyo ili awe sehemu ya kundi hilo.

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

5. Kudhihirisha UWANAUME wake; Pengine ni kwa imani potofu, marafiki, au tu kwa kumkomoa mpenzi wake, wanaume wengi huamua ku “cheat” kuonyesha tu yeye ni mwanaume wa shoka, na anaweza kufanya lolote, yaani yeye sio  “jinsia-mbili”.

6. Kutimiza Mahitaji yake anayoyakosa kwa mpenzi aliyenae hivyo kutafuta sehemu nyingine anayoona atapata.

7. Familia yake ni watu wa namna hiyo hii ni hatari; Kuna wanaume ambao ni wazinzi kwa kuwa tu baba yake, kaka zake, na watu aliolelewa nao wana tabia hii. Ni ngumu sana kumbadili mwanaume huyu.

8. Pombe,  na madawa ya Kulevya

9. Kumzoeza vibaya kwa maneno kama “Wewe iba tu lakini usikamatwe” Anahisi huwezi kumfanya chochote na utaizoea tabia yake hiyo

10. Kutaka kuona kama bado ana “uwezo” hasa kwa wanaume wenye Umri wa zaidi ya miaka 40.

MAKALA HII NA KUMI MUHIMU


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>