Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

RAIS KIKWETE AFUNGUA BARABARA YA DODOMA-FUFU

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiweka jiwe la msingi kuashiraia ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma- Iringa sehemu ya kutoka Dodoma - Fufu (Km70.9) huku akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa upande wa Tanzania Bi. Tonia Kandiero kushoto pamoja na Mwakilishi kutoka Serikali ya Japan na JICA, Ndugu Kuniaki Amatsu kulia huku Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akishuhudia tukio hilo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma- Iringa sehemu ya kutoka Dodoma - Fufu (Km 70.9) iliyojengwa kwa kiwango cha Lami. Wengine walioshika utepe ni Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania Bi. Tonia Kandiero, Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe pamoja na viongozi wengine.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


 Taaswira ya mkeka mpya kutoka Dodoma hadi Fufu wa Kilomita 70.9 aliouzindua Rais Kikwete
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wakimtazama Mwakilishi kutoka Serikali ya Japan na JICA Ndugu Kuniaki Amatsu na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania bi Tonia Kandiero walipokuwa wakipanda mti kama ishara ya kumbukumbu ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma- Fufu(Kilomita 70.9)
 Waziri wa zamani wa Ujenzi Mzee Job Lusinde akipanda mti kama ishara ya kumbukumbu ya ufunguzi wa rasmi wa barabara ya Iringa-Dodoma sehemu ya Dodoma-Fufu (Kilomita 70.9) huku Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli , Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge wakishuhudia tukio hilo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli  pamoja na viongozi wengine wakitaifa katika picha ya kumbukumbu mara baada ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma-Iringa sehemu ya Dodoma- Fufu Kilomita 70.9. Picha zote kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini –Wizara ya Ujenzi

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>