Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiongoza kikao cha kamati ya maandalizi ya sherehe ya miaka 4 ya Vijimambo ambayo imebeba ujumbe wa kutangaza maliasili na utalii wa Tanzania na kukemea Ujangili wa wanyama pori na misitu sherehe inayofanywa kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani pamoja na Jumuiya ya Watanzania DMV mgeni Rasmi atakuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiwa pamoja nae Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Mhe. Saidi Ali Mbarouk.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi Bwn. Baraka Daudi, Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Afisa Suleiman Saleh na Katibu wa Kamati ya maandalizi Bi. Asha Nyang'anyi wakiendelea na mkutano uliofanyika kwenye ofisi katika jengo la Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Washington, DC siku ya Jumanne Aug 26, 2014.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Afisa Ubalozi Suleiman Saleh na Bi Asha Nyang'anyi wakifuatilia mkutano.
Bwn. Baraka Daudi na Mhe. Balozi Liberata Mulamula wakifuahia jambo. Picha kwa hisani ya Vijimambo