Watu mia moja na ishirini wamenusurika kifo na wengine kujeruhiwa katika eneo la Kikatiti wilayani Arumeeru baada ya mabasi ya Hood lililokuwa linatoka Arusha kwenda Iringa kugongana na basi la Isamilo lililokuwa linatoka Moshi kuelekea mkoani Mwanza.
Wakizungumza baada ya kutokea ajali hiyo baadhi ya mashuda na abiria waliyokuwemo katika ajali hiyo wamesema dereva wa basi la Hood alikuwa katika saiti yake lakini ghafla lilitokea basi la Isamilo lililokuwa linalipita roli la mizigo kwenye kona kali pamoja na daraja ndipo likashinda na kuingia upande wa pili.
Raia wakishuhudia ajali ya basi la Hood ilivyotokea.
Kwa upande wake dereva wa basi la Hoodi ambaye pia ameumia mkono katika ajali hiyo amesema basi alililogongana nalo likuwa kwenye mwendo kasi ambao ulimshinda dereva kulimudu gari hilo huku alitoa wito kwa madereva wengine kuwa makini wanapo kuwa bara barani .
Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
CHANZO: ITV TANZANIA