Christian Bella
Na Josephat Lukaza
Msanii wa Muziki wa Dansi anayejulikana kama Christian Bella anayetamba na kibao chake cha Nani Kama Mama ni Mmoja wa Wasanii watakaotoa Burudani ya Kufa mtu katika Ukumbi wa Mlimani City Siku ya Jumamosi Tarehe 30 katika Fainali kubwa ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT).
Bella Amehaidi kutoa Burudani ya uhakika ambapo wapenzi wa muziki wake watafurahi na kufurahishwa na show atakayoitoa siku hiyo katika Fainali ya Kumkabidhi Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
Katika Fainali hiyo inayotarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Siku ya Jumamosi tarehe 30 huku viingilio vya Kuja kutazama fainali ya Kwanza kubwa vikiwa ni V.I.P Shilingi 50,000 na Kawaida 30,000 huku fainali hiyo ikirushwa live kupitia Kituo cha Runinga cha ITV na milango itakuwa wazi kuanzia Saa 7.30 Usiku.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Tanzania Movie Talents (TMT) ni shindano la Kwanza kufanyika Afrika Mashariki na Kati ambalo limeanzishwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd likiwa na lengo la Kuibua na Kusaka Vipaji vya kuigiza kwa watanzania ambao wana vipaji lakini walikosa fursa ya kuonekana. TMT ilianza Rasmi tarehe 1 April 2014 katika Mkoa wa Mwanza, Kanda ya Ziwa ambapo baadae shindano likaendelea katika Kanda nyingine Tano huku katika Kila Kanda Washindi walikuwa ni watatu huku kanda ya Pwani washindi walikuwa Ni 5 ambapo jumla ya Washindi 20 walipatikana na kuletwa Dar Es Salaam katika kambi na Hatimaye Mchujo kuanza na Kubakiwa na Washiriki 10 ambao leo hii wameingia Fainali ya kuzisaka zile Milioni 50 za Kitanzania.
Katika Fainali hiyo Kubwa kutakuwa na Burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.Sikiliza Moja ya Nyimbo atakazoimba Live Stejini Siku Hiyo ya Fainali