Baada ya uchunguzi wa kina katika benki kuhusu wizi wa fedha kwenye akaunti nne za abiria wa ndege ya Malaysia iliyopotea, hatimaye wezi wa fedha hizo wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.
Afisa mmoja mwanamke mwenye cheo cha juu katika benk ya Kuala Lumpur iliyotajwa kwa jina la HSBC, Nur Shina Kanan amekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuhamisha fedha katika akaunti tatu za abiria na moja ya mfanyakazi wa ndege ya Malaysia, MH370 na kumhusisha mumewe moja kwa moja katika wizi huo.
Bi. Nur Shina Kanan alifanya ujanja wa kibenki na kutumia cheo chake kujikopesha pesa hizo kinyume na taratibu za kifedha.
Ingawa mtu na mkewe walishitakiwa kwa makosa mengi, waliweza kuyakwepa makosa mengine 16 ikiwa ni pamoja na makosa ya kukaidi amri ya mahakama.
CHANZO: BBC SWAHILI