Rapper Ilunga Khalifa aka Cpwaa amedai kuwa video yake ya Chereko Chereko iliyoongozwa na Adam Juma bado inafanyiwa marekebisho.
Cpwaa amesema video hiyo ikitoka watu wataona jinsi ilivyo tofauti na kwamba hakuna video kama hiyo kuwahi kufanyika nchini.
“Video inafanyiwa marekebisho pia nilikuwa ninasubiri watu wote watoe video zao, kama Vanessa, Diamond, akina Shetta, akina Jux, kwahiyo video inafanyiwa marekebisho na itatoka inshallah wiki hii,” amesema Cpwaa.
“Kikubwa ambacho nimekifanya nimefanya video ambayo haijawaHi kutokea Tanzania na haitajirudia, ingawa video yangu imepitwa na muda lakini ni video ambayo itabiki milele. Mpango mzima baada ya kuachia video wiki moja baadaye nitaachia tena wimbo mpya ambayo nimefanya na P.Funk. Video hii itakuwa tofuti, watu wengi huwa wanakimbia nje ambapo mimi nilishafanya sana, lakini mimi nimeamua kwenda South Africa sio kutumia director wa South Africa nimetumia director wetu Adam Juma. Kwahiyo ninachosema ni kwamba lazima tuthamini vya nyumbani location, culture, lugha na madirector na kila kitu, lazima tuanze nyumbani kwanza ndio mpango mzima. Video yangu Chereko Chereko ikitoka itaonyesha namna gani ninasema uzalendo huanza nyumbani na nyumbani tunaweza.”
CHANZO: BONGO 5