Mtangazaji wa Clouds fm, Ephraim Kibonde na Gadner G Habash Wakiingia katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
NA Mwandishi Wetu
WATANGAZAJI wawili, akiwemo Ephraim Kibonde (42) wa Kituo cha Redio cha Clouds fm, leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, kujibu mashitaka mawili, likiwemo la kumtukana ofisa wa polisi.
Wakisomewa mashitaka hayo mbele ya ya Hakimu Mfawidhi, Anicieta Wambura, Wakili wa Serikali Salum Ahamed, alidai kuwa mnamo Agosti 9, mwaka huu, katika Kituo cha Polisi Oysterbay, wilaya ya Kinondoni, washtakiwa Kibonde (42) na Gardner Habash (41), walimtukana tusi la nguoni ofisa wa polisi kituoni hapo mwenye namba E 884 SGT, Silyvester.
Kibonde, anadaiwa siku hiyo katika maeneo ya Bamaga, alikataa kutii amri halali aliyopewa na polisi ya kutakiwa kurudisha gari eneo la tukio baada ya ajali.
Ilidaiwa kuwa mshitakiwa alikataa kutii amri hiyo, badala yake alikimbiza gari hadi alipokamatwa eneo la Ubungo kwenye mataa.
Washitakiwa hao waliachiwa kwa dhamana hadi Septemba 10, mwaka huu, kesi itakapotajwa ambapo kila mmoja alitakiwa kuwa na wadahamini wawili waliotia saini bondi ya sh.500,000.
Katika hatua nyingine, Kibonde alipandishwa kizimbani tena mbele ya hakimu huyo, akikabiliwa na mashitaka mawili ya kuendesha chombo cha moto akiwa amelewa.
Ahmed alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo Agosti 9, mwaka huu, maeneo ya Makumbusho, barabara ya Bagamoyo.
Alidai kuwa mshitakiwa alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T.759 CPM aina ya Toyota kwenye barabara ya umma akiwa katika hali ya ulevi kwa kipimo kilichopindukia cha ML 190.9.
Pia alidaiwa katika eneo hilo, alikuwa akiendesha kizembe gari huku akishindwa kuacha nafasi kwa magari mengine na kugonga gari lenye namba za usajili T.960 CBB aina ya Hyundai Tucon.
Wakili huyo alidai tukio hilo lilisababisha uharibifu wa gari la mshitakiwa na lingine lenye namba za usajili T.960, Mshitakiwa alikana mashitaka na kuachiwa kwa dhamana hadi Septemba 9, mwaka huu, kesi itakapotajwa baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili waliotia saini bondi ya sh.milioni nne kila mmoja.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI