Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

PICHA: ABIRIA WANUSURIKA KIFO BAADA YA GARI KUPARAMIA KITUO

$
0
0
 Gari aina ya Toyota Raum lenye namba za usajili T483 CMU likiwa eneo la kituo cha mabasi.
ABIRIA waliokuwa katika kituo cha mabasi eneo la Quality Plaza jijini Dar wakisubiri usafiri wamenusurika kifo baada ya gari aina ya Toyota Raum lenye namba za usajili T483 CMU, kuhama njia katika barabara ya Nyerere na kuparamia kituo hicho.
 Dereva wa gari lililopata ajali ambaye jina lake halikufahamika mara moja akiongea na simu baada ya kunusurika kifo.
Dereva wa gari hilo mwenye asili ya Kihindi ambaye jina lake halikufahamika mara moja alishindwa kulimudu ndipo lilipovuka ukingo unaotenganisha barabara hiyo na kuhamia upande wa pili kisha kuparamia kituo cha abiria. Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa

ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 Tairi likiwa limepasuka baada ya ajali hiyo.
Mashuhuda wakiwa eneo la tukio.
PICHA NA GPL

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>