Ndege inayomilikiwa na kampuni ya Taban Air imeripotiwa kuanguka katika makaazi ya watu Jumapili (Agosti 10) baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Mehrabad Maghribi mwa mji wa Tehran. TV ya taifa ya Iran imesema watu wote 40 wamepoteza maisha katika ajali hiyo na uchunguzi umeanza kufanywa ili kubaini chanzo.
Ndege hiyo iliyojulikana kwa jina la Iran 141 ilitengezwa nchini Iran kupitia teknologia ya Ukraine. Iran imekabiliwa na ajali kama hizo katika siku za hivi karibuni kutokana na ndege zake zilizozeeka mbali na marekebisho mabaya inazozifanyia
Source: BBC