Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

MAGUFULI AKAGUA UJENZI WA KIVUKO CHA MSANGAMKUU (MV. MTWARA), DARAJA LA KIGAMBONI PAMOJA NA UKARABATI WA KIVUKO CHA MV. KIGAMBONI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipanda ngazi katika Kivuko cha Msanga Mkuu MV Mtwara kwa ajili ya kufanya ukaguzi wake leo mjini Dar es Salaam. 
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wa kwanza kulia akipewa maelezo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe kuhusu ujenzi wa kivuko cha Msanga Mkuu(MV Mtwara) kilicho katika hatua za mwisho za matengenezo chini ya Kampuni ya Sangoro Marine Transpot Limited. 


ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Mratibu wa Mradi wa Daraja la Kigamboni kutoka NSSF Mhandisi Karim Mataka wa kwanza kutoka kulia akitoa Maelezo ya maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni kwa Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli wakati wa ukaguzi wa Daraja hilo jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mratibu wa Mradi wa Daraja la Kigamboni kutoka NSSF Mhandisi Karim Mataka pamoja na viongozi wengine kutoka Wizara ya Ujenzi wakiendelea na ukaguzi wa daraja la Kigamboni kama inavyoonekana. 
Luteni Kanali Abel Gwanafyo akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ukarabati wa Kivuko cha MV. Kigamboni kinachofanyiwa ukarabati na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kupitia kikosi cha Wanamaji (Nav) Kigamboni jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika kivuko cha MV. Kigamboni mara baada ya Ukaguzi. 
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kulia akizungumza na wakazi wa Kigamboni kuhusu ukarabati wa Kivuko cha MV Kigamboni. Dkt. Magufuli aliwasihi wananchi hao kuwa wavumilivu kwani baada ya wiki mbili Kivuko hicho kitakuwa tayari kwa kazi ya kuwavusha watu kama kawaida. 
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisubiri Kivuko cha MV Magogoni kwa ajili ya kuvuka mara baada ya kuzungumza na wakazi wa Kigamboni kuhusu ukarabati wa Kivuko cha MV Kigamboni. 
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipanda kwenye kivuko cha MV Magogoni mara baada ya kuzungumza na wakazi wa Kigamboni kuhusu ukarabati wa Kivuko cha MV Kigamboni jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akitoka kwenye kivuko cha MV Magogoni mara baada ya kuvuka kutoka Kigamboni alipowahutubia wakazi wa Kigamboni kuhusu ukarabati wa Kivuko cha MV Kigamboni jijini Dar es Salaam. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>