Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

WATU WATANO (5) MBARONI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MADEREVA WAWILI WA BODABODA MKOANI DODOMA

$
0
0

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP

Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu watano (5) kwa kuhusika na mauaji ya madereva wawili wa bodaboda kwa nyakati tofauti.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema watuhumiwa watatu ambao ni ALEX S/O LETEMA LEWENJE mweye umri wa miaka 20, Mkaguru, ANDREA S/O MAJUTO CHIGUNDULA mwenye umri wa miaka 24, Mkaguru na NABAKI S/O MAUNGO MWIGOE mwnye umri wa miaka 23, Mkaguru wote wakazi wa Gairo Mkoa wa Morogoro ambao wanashikiliwa kwa tuhuma za kumwuua JACKSON S/O JOHN MASAUSE tarehe 01/07/2014 huko katika Kijiji cha Lenjulu, Tarafa ya Mlali Wilayani Kongwa kisha kuchimba shimo na kumfukia na kupora pikipiki yenye namba za usajili T. 374 CXH aina ya FEKON pamoja na simu yake.

Pia Kamanda MISIME amesema watuhumiwa hawa baada ya kukamatwa walikiri ni kweli walimkodi marehemu tarehe 01/07/2014 na wakaenda kuonyesha walikoficha pikipiki hiyo na simu huko Gairo. Mwili wa marehemu uligundulika tarehe 01/08/2014 na shoka walilotumia kumpiganalo kichwani lilikutwa pembeni ya sehemu walipo mfukia marehemu.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Kamanda MISIME ameongeza kuwa watuhumiwa wengine ni ALLY S/O NURDIN ITEKULE mwenye umri wa miaka 25, Mrangi pamoja na HALIFA S/O JUMA MSALA mwenye umri wa miaka 28, Mrangi wote wakazi wa Swaswa Dodoma Mjini na Kondoa ambao wanatuhumiwa kumkodisha dereva wa bodaboda MARTIN S/O VICTORY MKORO mwenye umri wa miaka 22, Msandawe Mkazi wa Njedengwa tarehe 26/07/2014, kisha kumuua kwa kumkata na kitu chenye ncha kali shingoni na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili kisha kupora pikipiki yenye namba za usajili T. 777 CPR ambayo ilipatikana baadaye. Tukio hilo walilifanya katika eneo la Njedengwa karibu na makaburi ya Chaduru.

Watuhumiwa walikamatwa wakiwa huko Kidoka katika Wilaya ya Chemba wakiuza pikipiki nyingine yenye namba za usajili T. 372 CHF aina ya Boxer wailiyoipora tarehe 27/07/2014 na walikiri kumuua MARTIN S/O VICTORY MKORO pia walifanya hivyo kwa sababu alikuwa anawafahamu ili asije akawasema lakini wakasahau kuwa mkono wa dola ni mrefu. Watuhumiwa hawa wanahojiwa pia kwa matukio mengine ambayo wamekiri kuhusika na uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Aidaha Kamanda MISIME amesema mtandao huu wa watuhumiwa hawa umegundulika kutokana na ushirikiano mzuri wa wananchi. Polisi Mkoa wa Dodoma wanawashukuru sana wananchi kwa ushirikiano huo.

Kamanda MISIME ametoa wito pia kwa wahalifu kuwa uhalifu haulipi hivyo wabadilike na kuwa wananchi wema wanaochukia uhalifu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles