Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe Mohammed Dewji (MO), akizungumza kwenye hafla hiyo ya utiliaji saini wa mkopo wa bilioni 100 za kitanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu akizungumza kwenye hafla ya utiliaji saini wa mkopo wa bilioni 100 za kitanzania baina ya benki yake na kampuni ya MeTL mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
.MetTL yajipanga kupanua soko lake la mafuta Afrika Mashariki na Kusini
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya Mohammed Enterpries Tanzania Limited (MeTL GROUP) kupitia kampuni yake dada ya kuingiza, kuhifadhi na kusambaza mafuta nchini ya Star Oils Ltd. imepata mkopo wa bilioni 100 kutoka kwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya hafla ya utiliaji saini wa mkopo huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu na Mbunge wa Singida Mjini, Mhe, Mohammed Dewji (MO) amesema mkopo huo utafungua mianya zaidi kwa kampuni ya Star Oils kusambaza mafuta nje na ndani ya nchi.
Amesema kwamba baada ya majadiliano ya muda mrefu kati ya timu ya wataalamu kutoka MeTL makao makuu na maafisa wa NBC kutoka nchini na Afrika Kusini wamefikia makubaliano ya kupata mkopo huo mkubwa na wa aina yake katika sekta ya mafuta hapa Tanzania.
Amesema kwamba kampuni ya Star Oils ina mipango ya kusambaza mafuta katika nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa jangwa la Sahara ikiwa ni sehemu ya mikakati yake ya kujipanua kibiashara ndani na nje ya Afrika.
"Mpango huu utaiwezesha Star Oils kupanua malengo yake katika soko la kimataifa ikiwa ni pamoja na kukuza uzalishaji na usambazaji wake katika ngazi ya Afrika Mashariki na Kusini mwa jangwa la sahara," amesema MO.
MO aliongeza kuwa hatua ambayo kampuni hiyo imefikia ni kubwa kwa kuonyesha dhamira ya kuwekeza na kufanya biashara ya mafuta Afrika mashariki na kusini mwa jangwa la sahara.
"Mkopo huu utasaidia kampuni ya Star Oils kuongeza uzalishaji na usambazaji wa mafuta ya kwenye soko la Afrika mashariki na kusini mwa Afrika,”
Mkuu wa Idara- Huduma za Kibenki kwa Wateja wakubwa na Uwekezaji wa NBC, Andre Potgieter akizungumza na wageni waalikwa kwa kutaja shughuli mbalimbali na bidhaa huduma za benki hiyo.
"Sisi tuna mipango ya kuanza kusambaza mafuta na bidhaa za Petroli katika nchini za Kusini mwa Afrika kama sehemu ya jitihada za kampuni za kupanua biashara zake katika soko la Afrika," amesema.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Star Oils Ltd, Nazir Haji amesema kwamba mkopo huo utachochea chachu ya uzalishaji, uhifadhi na usambazaji wa mafuta na kusukuma maendeleo ya sekta mafuta nchini.
Amesema kwamba kampuni ya Star Oils inajipanga kufanya biashara ya mafuta kuwa endelevu hapa nchini na Afrika mashariki ili uchumi wa nchi za Afrika mashariki ziweze kukua kwa kutegemea tija ya uzalishaji wa mafuta.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu amesema kuwa benki hiyo inahitimisha safari ya majadiliano na kampuni mama ya Star Oils, Mohammed Entrepries Tanzania Limited (MeTL GROUP) ya mkopo wa bilioni 100.
"Star Oils ni kampuni dada ya METL ni moja ya makampuni yanayokwenda kasi katika biashara ya ushindani katika Afrika Mashariki na Kusini mwa jangwa la sahara na rekodi yao ya mauzo na biashara ni ya kuridhisha," amesema.
Mkuu wa Idara- Huduma za Kibenki kwa Wateja wakubwa na Uwekezaji wa NBC, Andre Potgieter akionyesha toleo la jarida la "THE AFRICA REPORT" lilioandika mafanikio ya kampuni ya MeTL GROUP zilizomvutia zaidi na kupelekea kuwa na imani na kampuni hiyo na kuamua kufanya biashara nao.
Aliongeza kwamba METL ni moja ya makampuni yalionyesha rekodi nzuri katika biashara ya viwanda, nguo, vinywaji, bima na mafuta na wanastahili kuwezesha kwa kupata mikopo mikubwa na ya muda mrefu kupitia taasisi za kifedha nchini na nje ya nchi,”
"Sisi kwenye benki ya NBC tunayofuraha kubwa kwa kupata nafasi ya kufanya biashara na moja ya makampuni yanayokuja kwa kasi katika bara la Afrika na vile vile NBC ni benki ambayo ipo tayari kusaidia wateja wake,” aliongeza
Bi. Melu alisisitiza kuwa baada ya NBC kuridhisha na shughuli za kibiashara na mzunguko wa fedha wa MeTL wameamua kutoa mkopo huo ili waweze kupanua biashara yao katika masoko ya kimataifa.
Star Oils kwa sasa inatekeleza awamu ya pili ya mradi mkubwa wa kuhifadhi mafuta ya Petroli na baadaye kujenga usambazaji wa mafuta nchi nzima kwa njia ya mlolongo wa vituo vya karibu 200 vya Petroli nchini.
Mkuu wa Idara- Huduma za Kibenki kwa Wateja wakubwa na Uwekezaji wa NBC, Andre Potgieter akipeana mkono wa pongezi na Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe, Mohammed Dewji.
Uwezo wa jumla ya uhifadhi wa kituo hiki juu ya kukamilisha mradi itakuwa lita 68 milioni, kuundwa tu kwa ajili ya kuhifadhi ya Petroli, Gesi Mafuta na mafuta ya taa. Wingi wa bidhaa hizi kwa sasa ni kuuzwa kwa misingi ya jumla na mipango ya baadaye soko lao kupitia vituo vya METL Group vya rejareja vya petroli.
NBC imetiliana saini ya mkopo wa shilingi za kitanzania bilioni 100 na kampuni ya kusambaza mafuta ya jijini Dar es Salaam, Star Oils Ltd katika mpango mkakati wa kuendeleza sekta ya mafuta nchini.
Picha juu na chini ni Baadhi ya wafanyakazi wa makampuni ya MeTL GROUP na Benki ya NBC waliouhudhuria hafla hiyo ya utiliaji saini wa mkopo baina MeTL na NBC.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu na Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe Mohammed Dewji wakitiliana saini ya mkopo huo wa bilioni 100 za kitanzania.
Makamu wa Rais wa Makampuni ya MeTL GROUP, Vipul Kakad (wa pili kulia walioketi) na Mkuu wa Idara- Huduma za Kibenki kwa Wateja wakubwa na Uwekezaji wa NBC, Andre Potgieter wakiweka saini zao kwenye mkataba huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu na Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe Mohammed Dewji wakibadilishana hati za mkopo huo katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja baina ya MeTL GROUP na NBC baada ya utiliaji saini wa mkopo huo.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara- Huduma za Kibenki kwa Wateja wakubwa na Uwekezaji wa NBC, Andre Potgieter, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu, Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe Mohammed Dewji, Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Vipuk Kakad na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni dada ya MeTL GROUP Star Oils Ltd, Nazir Haji kwenye picha ya pamoja.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni dada ya MeTL GROUP Star Oils Ltd, Nazir Haji akitoa shukrani zake kwa NBC.
Makamu wa Rais wa Makampuni ya MeTL GROUP, Vipul Kakad (katikati) na wasaidizi wa Mheshimiwa Mohammed Dewji kwenye hafla hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe Mohammed Dewji akimwonyesha kitu kwenye simu yake ya kiganjani Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu wakati wa hafla hiyo.
Wafanyakazi wa NBC na MeTL Group wakibadilishana mawazo wakati wa hafla hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe. Mohammed Dewji (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu (kulia), Mwanasheria Mkuu wa MeTL GROUP, Zakia Riyaz Ali (wa pili kulia), na Vikash KG wa Star Oils Ltd wakati wa hafla hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe Mohammed Dewji akifurahi jambo na mmoja wa wafanyakazi wa NBC wakati wa hafla hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mhe Mohammed Dewji akiteta na wafanyakazi wa NBC kwenye hafla hiyo.