Mchezaji wa Taifa Stars, Shomari Kapombe akilia kwa uchungu baada ya Stars kupoteza nafasi ya kucheza hatua ya makundi kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Afrika 2015
Timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jana iliondolewa rasmi kwenye michuano ya kuwania kufuzu kucheza kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 kwa kufungwa mabao 2-1 na Msumbiji aka The Mambas.
Kichapo hicho kiliwafanya baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars akiwemo Shomari Kapombe kulia kama watoto wadogo.
Mbwana Samattah akishindwa kuzua kilio baada ya Taifa Stars kufungwa
“Taifa Stars imecheza mechi nyingi ambazo nimehudhuria, ndani na nje ya nchi. Sijaona wachezaji wakitokwa machozi kama Jana. Ndani ya chumba cha kubadilisha nguo niliona uchungu na machozi ya vijana wetu. Kwa pamoja walikuwa wanasema ‘nyumbani kama ugenini, ugenini ugenini’. Somo kubwa sana hilo,” ameandika Zitto Kabwe.
Una maoni gani kuhusiana na kikosi cha Taifa Stars?
Picha: KiliLager.com