Hiki ni kisa kilichotokea nchini Kenya na kuripotiwa na NTV, ambapo mwanamke mmoja ambaye ni mama ameamua kumfunga mwanaye kama mzigo na kumtuma kwa baba yake kwa njia ya kifurushi. Mtoto huyo wa kiume ana umri wa wiki tatu.
Wafanyakazi wa kampuni ya G4S ambapo anayedaiwa kuwa baba wa mtoto huyo nafanya kazi, wamesema walikuta kifurushi ambacho hawajawahi kupokea kimetelekezwa nje ya ofisi zao na walipofungua kibox wakakuta ni mtoto amefungwa kama mzigo.