Watoto wakiwa wanaangalia vitu vya ndani vilivyokusanywa pembeni mwa nyumba iliyobomolewa na Tingatina la Mamraka ya ustawishaji makao makuu (CDA) ambapo jumla ya nyumba 18 zilibomolewa katika kitongoji cha Msangalale kata ya makulu Manispaa ya Dodoma.
Wakazi wa kitongoji cha Msangalale kata ya Makulu Manispaa ya Dodoma wakiwa wamekaa chini ya mti kwa huzuni pamaoja na samani za ndani ya nyumba zao muda mfupi baada ya nyumba hizo kubomolewa na Tingatinga la Mamlaka ya ustawishaji wa mji wa Dodoma (CDA)
Mifuko ya karanga na mazao mengine pamoja na samani za ndani zikiwa zimeangukiwa na kifusi cha nyumba iliyobomolewa na Tingatinga la (CDA) waliowataka kuhama ili kupisha Barabara.