Katika kuunga mkono jitihada za kupunguza ajali barabarani,wakali katika muziki wa bongo fleva Mr Blue, Amini, Banaba Boy na Dyna Nyange wamerekodi wimbo wa pamoja kuhamasisha uzingatiaji wa usalama barabarani na kwenye vyombo vya usafiri. Wimbo unaitwa Dereva Makini umetayarishwa na katika studio za C9. Kampeni hiyo ya dereva makini imeandaliwa na Transevents Marketing ambao ndio wamiliki wa tovuti ya Kariakoo Digital kwa lengo la kutoa hamasa kwa madereva kuwa makini wanapoendesha magari ili kuwawezesha abiria kufika salama waendako.
↧