Baadhi ya washiriki wa Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakiwa mbele ya Majaji tayari kwa kupewa maoni yao na hatimaye kutaja watakaotoka chomwa na jua la utosi kwa Wiki hii. Kutoka Kulia ni Tishi Abdallah, Katikati ni Mtawa Kapalata na Kushoto ni Joshua Wambura.
Anneth Peter (katikati) akiwa mwenye huzuni kubwa kutokana na Mshiriki mwenza kutoka kanda ya Kaskazini Kareb John (hayupo pichani) kutoka kwenye shindano mara baada ya kuchomwa na jua la utosi.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Washiriki wawili waliondolewa katika Shindano kwa wiki hii wakiwa mbele ya Jukwaa mara baada ya kutangaziwa kushindwa kuendelea kutokana na kuwa na idadi chache ya kura kutoka kwa watazamaji.Wa kwanza kushoto ni Kareb John na Malima Deogratius ambao wameaga mashindano
Kareb John na Malima Deogratius mara baada ya kutangaziwa kuyaaga mashindano..
Mara baada ya Kareb John Kuaga mashindano Mshiriki kutoka kanda ya Kaskazini Annet Peter alionekana mwenye huzuni kubwa
Washiriki wakiwa na huzuni kutokana na wenzao kuaga mashindano.Picha zote na Josephat Lukaza wa Proin Promotions, Dar Es Salaam
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam.
Ni wiki ya Pili sasa ya mchujo katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo washiriki wengine wawili wamechomwa na Jua la Utosi na hatimaye kuaga shindano. Mchujo huo ni muendelezo wa Mchujo ambao kila wiki washiriki wawili watachomwa na jua la utosi na hatimaye kupelekea kuaga shindano la TMT.
Mpaka sasa Washiriki wanne tayari wameshayaaga mashindano na kupelekea washiriki 16 kubakia katika mchujo unaofuata.
Mpaka sasa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limekua ni shindano lililoteka hisia za watanzania wengi waliopo ndani na nje ya Nchi kutokana na ubora, Uhalisia na Ubunifu wa hali juu kutoka kwa Waandaaji na waendeshaji pamoja na washiriki kuonyesha Vipaji vyao.
Ili kuweza kumnusuru mshiriki wako asichomwe na Jua la Utosi unachotakiwa ni kumpigia kura kadri uwezavyo ili kumfanya abaki ndani ya Nyumba ya TMT.
Mara baada ya washiriki wa wiki hii kuondolewa katika shindano hali imezidi kuwa ni simanzi kwa washiriki kutokana na kutokujua ni zamu ya nani kutoka wiki ijayo.
Washiriki waliotoka wiki hii ni Kareb John ambae alikua mmoja kati ya Washindi watatu kutoka kanda ya Kaskazini Mkoani Arusha huku Mshiriki Malima Deogratius akiwa ni Mshindi kutoka KAnda ya Pwani Mkoani Dar Es Salaam.
Ili kuweza kumnusuru mshiriki umpendae unachotakiwa kufanya ni Kuandika neno "TMT" ikifuatiwa na namba ya Mshiriki halafu unatuma kwenda namba 15678. Mfano TMT00 tuma kwenda 15678. Piga kura kadri uwezavyo ili kumnusuru mshiriki wako kutochomwa na Jua na Utosi wiki ijayo.
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ni shindano lililobuniwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited ambayo inahusika na utengenezaji, Usambazaji na Uuzaji wa filamu za Kitanzania huku ikiwa na malengo pia ya Kuibua vipaji vya Kuigiza na Mpira wa Miguu kwa Wanawake. Shindano hili Pia linaendeshwa na Kusimamiwa pia na Kampuni bora ya Usambazaji wa Filamu nchini ya Proin Promotions Limited
Huzuni na Simanzi zaendelea kutawala ndani ya Nyumba ya TMT kwa washiriki hao wawili kuondoka lakini Pia Hofu Yaendelea Kutanda ndani ya Nyumba ya TMT kwa washiriki kwa kutokujua ni zamu ya nani sasa kuchomwa na jua la utosi litakalompelekea kuaga shindano kwa wiki ijayo.