Shirikisho la soka duniani FIFA limeondoa marufuku lililoiwekea Nigeria isishiriki mashindano yoyote ya kimataifa.
Shirikisho hilo lilikuwa limeipiga marufuku Nigeria kutoshiriki katika michuano yoyote ya soka ya kimataifa mapema mwezi huu kwa kuwa serikali ya Nigeria iliingilia uongozi wa shirikisho hilo nchini Nigeria.
FIFA imeamua kuchukua uamuzi wa kuondoa marufuku hiyo baada ya mahakama kuondoa agizo la kuwatoa baadhi ya maafisa wakuu wa shirikisho hilo nchini Nigeria.