Watu duniani kote Ijumaa hii wanasherehekea, “Mandela Day” ikiwa ni ya kwanza tangu rais huyo wa kwanza wa Afrika Kusini afariki dunia. Kama angekuwa hai, leo angetimiza umri wa miaka 96.
Kwa miaka mitano sasa mamilioni ya watu duniani wamekuwa wamekuwa wakijitolea dakika 67 za muda wao kila July 18 kuadhimisha miaka 67 ya harakati za kupigania uhuru za Mandela nchini Afrika Kusini. Mandela alifariki December 5 mwaka jana akiwa na miaka 95 kutokana na kuugua kwa muda mrefu.
Shughuli mbalimbali za kusherehekea Mandela Day zitafanyika katika miji ya Paris, New York, Dallas, London, Edinburgh na Glasgow, wakati filamu iliyoigiza maisha yake ikioneshwa China.