Vijana wa JembeniJembe wa Skylight Band wakitikisa jukwaa kutoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo Ijumaa iliyopita kwenye viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar.
Digna Mbepera, Mary Lucos na Sony Masamba wakiwajibika jukwaani.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Aneth Kushaba AK47 akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar.
So how do you expect me to live alone with just me ...'Cause my world revolves around you
It's so hard for me to breathe...No air ...air...Bonge moja la Kolabo ni Sam Mapenzi na Aneth Kushaba AK47 wakitoa burudani.
It's so hard for me to breathe...No air ...air...Bonge moja la Kolabo ni Sam Mapenzi na Aneth Kushaba AK47 wakitoa burudani.
Vijana watanashati, nadhifu wanastahili kila sifa kupewa wao....si wengine ni wa Skylight Band ambayo ndio habari ya mujini kwa sasa haina mfano wake...Divas wa bendi hiyo Kutoka Kulia Digna Mbepera, Mary Lucos na Aneth Kushaba AK47 wakipewa sapoti na mkongwe wa muziki wa dansi nchini Joniko Flower Ijumaa iliyopita.
Sam Mapenzi akiongoza kutoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita huku akipewa back vocal na Joniko Flower, Hashim Donode na Sony Masamba ndani ya viunga vya Thai Village.
Taratibu mdogo mdogo amsha amsha hiyo kwa raha zetu......Njoo ujinafasi kwenye viunga vya Thai Village na Skylight Band leo usiku kuanzia saa tatu.
Mary Lucos akiwaburudisha mashabiki wa Skylight Band huku akisindikizwa na Digna Mbepera Ijumaa iliyopita.
Sugua sugua mpaka kitakate....! Unakaribishwa usiku wa leo usugue kiatu chako na SKYLIGHT BAND ndio habari ya mujini kwa sasa!
Mashabiki nao hawakubaki nyuma mule mule tu kama inavyoonekana pichani.
Mguu wa kushoto mbele wa kulia nyuma......!
Ya chuma chuma nataka mukanda ya Chuma chuma.....! mashabiki waliofuzu kucheza moja ya style za Skylight Band....Njoo na wewe leo tujumuike pamoja.
PICHA HII ITAKUWA USHAHIDI TOSHA: Mmoja wa mashabiki wa Skylight Band ambaye jina lake halikuweza kupatikana akionyesha uwezo wake wa kusakata ma-style mbalimbali ya bendi hiyo baada ya Joniko Flower kuvutiwa na uchezaji wake kama inavyoonekana pichana jamaa alivyo COPY na KU-PASTE miondoko hiyo.
KWANINI TUANDIKIE MATE WAKATI WINO UPOOO...? Hebu jione mwenyewe utafikiri hawa jamaa mapacha mpaka Style ya kuweka vidole jamaa kaiga.
Joniko Flower alichemka na kuamua kumshangaa tu jamaa anavyosakata mangoma...Wewe Je unakipaji kama hichi...? Basi usikose Ijumaa ya leo uje utuonyeshe ufundi wako, na SKYLIGHT BAND wanazawadi maalum ikiwemo usafiri wa bure wa kukurudisha nyumbani kwako na vingine kibao kwa shabiki atakayesakata miondoko kama hii jukwaani.
Aneth Kushaba AK47 mwenye alisalimu amri kwa huyu jamaa....!
Birthday Girl Renatha Mushi akifurahi burudani ya Skylight Band na wadogo zake wapendwa walioamua kumfanyia surprise ya nguvu.
Baadhi ya members wa WANAMANYOYA wakijumuika na mashabiki wa Skylight Band kuonyesha style mbalimbali za uchezaji wao.
Hiki ni kiungo muhimu sana katika muziki wa LIVE Band....Idrissa Drum alihusika kupika ladha nzuri ya muziki wa Skylight Band.
Kikuku huyo ana manyoya huyooo......Dunda dunda pasua twende...!
Mashabiki wa Skylight wakicheza na kupiga mayowe ya furaha kutokana na kukunwa na burudani nzuri ya bendi hiyo.
Kumbe ni Aneth Kushaba AK47 ndio alikuwa akiwachizisha mashabiki wa Skylight Band kwenye show ya aina yake Ijumaa iliyopita ndani ya viunga vya Thai Village.
Mambo ya mduara yalikhusika pia Ijumaa iliyopita ndani ya viunga vya Thai Village leo pia kama kawaida tupo hapo kuanzia saa tatu usiku....No where else to go rather than SKYLIGHT BAND...JUST FOLLOW THE LIGHT!
Kinyau nyau kikiacha Pweza....!Eeeeh mambo ya pwani hayo shurti ulegeze vidole ndio raha yake ati....! Joniko Flower akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band.
WANAMANYOYA wakipata Ukodak na Birthday Girl dada yetu mpendwa kabisa Renatha Mushi aliyetimia miaka kadhaa hivi na kuja kusheherekea na Skylight Band.
Divas wa Skylight Band Mary Lucos na Digna Mbepera wakipata Ukodak na wadau wa ukweli wenye mahudhurio ya kuridhisha kila Ijumaa ndani ya kiota cha Thai Village.
Mratibu wa Skylight Band Lubea akishow love na mdogo wake All the way from Zanzibar....!
Back stage.
Mmoja wa Masuperstar anayeunda kundi la Wadananda akipata Ukodak na mremboz mkareeee!!
Baadhi ya mashabiki wa Skylight Band wakipata Ukodak wa nguvu.
Wamependeza hawajapendeza.