Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP akielekeza jambo katika ukaguzi wake
Mkaguzi wa Tarafa ya Goima A.Insp Msika akisoma taarifa kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wananchi wa Tarafa ya Goima wilaya ya Chemba mkoani Dodoma wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP
Kamanda MISIME kushoto akifuatiwa na OCD Chemba Vicent Chua - SSP, OC-CID Lutha na Mkaguzi wa Tarafa Yuda akiongea jambo katika tarafa ya Kwamtoro Wialayani Chemba Dodoma
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP akiongea na viongozi na wananchi wa tarafa ya Farkwa Wialaya ya Chemba Mkoa wa Dodoma
Wananchi wa Tarafa ya Farkwa Wialaya ya Chemba Dodoma wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVI MISIME – SACP amewataka viongoz wa Tarafa za Farkwa, Kwamtoro, Mondo na Goima Wilayani Chemba Mkoani Dodoma kushirikiana na Jeshi la Polisi kuielimisha jamii kuanzia ngazi ya familia kwa kuwaeleza kuwa matatizo na migogoro iliyopo ndani ya jamii haitatuliwi kwa kujichukulia sheria mikononi bali ni kwa kufanya majadiliano ndani ya vikao katika ngazi mablimbali na kufikia mafanikio.
Aliyasema hayo Wilayani Chemba alipokuwa akitembelea tarafa nne za Wilaya hiyo (Farkwa, Kwamtoro, Mondo na Goima ) ili kuongea na viongozi wa tarafa hizo na kutoa elimu ya Polisi jamii pamoja na kuwakabidhi rasmi wakaguzi wa tarafa na Polisi kata ili waweze kushirikiana nao kutoa elimu kwa jamii juu ya utii wa sheria bila shuruti, kujenga familia zisizokuwa na mhalifu na kubaini viini vya uhalifu, vurugu na migogoro katika maeneo yao.
Kamanda MISIME amewaeleza maana ya Polisi jamii kuwa ni ushirikishwaji wa kila mtu katika jamii kulingana na nafasi yake ili kuleta amani, utulivu, usalama na ustawi wa jamii, hivyo jamii inapaswa kushiriki katika suala la ulinzi na usalama.
Aidha Kamanda MISIME amesema viongozi wanatakiwa kuimarisha kamati za ulinzi na usalama za tarafa, kata, vitongoji, vijiji, mitaa na hata katika maeneo ya ibada lakini pia kuzitambua rasilimali za kiuchumi, kuzilinda na kuheshimu mipaka ili kuweza kutatua kero za mbalimbali za wananchi.
Pia aliongeza kwa kusema malengo makubwa ya Polisi jamii ni kuweka mazingira ya ushirikiano wa dhati kati ya Polisi na wananchi ili jamii ipate ujasiri iweze kukemea, kufichua, kuzuia uhalifu na kutatua migogoro kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo pamoja na kujenga utayari wa kuchukia uhalifu. Vilevile kuwa tayari kutoa ushahidi wa kile walichoona wakati tukio la kiuhalifu lilipotokea.
Pamoja na hayo aliwapongeza wananchi kupitia viongozi wa tarafa hizo kwa kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi ambavyo vimesaidia kupunguza uhalifu na aliwataka waendelee kuimarisha na kuunda vikundi vingine vipya.
Nao viongozi mbalimbali wa tarafa hizo wakiwemo Maafisa tarafa, Madiwani wa kata, Maafisa ugani, Watendaji wa kata na tarafa, wenyekiti wa Serikali za mitaa, Viongozi wa dini, Wazee maarufu wa kata na tarafa pamoja na viongozi wa vikundi vya ulinzi shirikishi wamemshukuru Kamanda MISIME kwa kuweza kufika kwenye tarafa hizo na kuzungumza nao namna ya kushirikisna na Polisi katika kuimarisha ulinzi ili kupunguza uhalifu katika tarafa hizo na kusema kuwa elimu waliyoipata wataifanyia kazi kwa kuelimisha jamii juu ya ulinzi na usalama katika jamii inayowazunguka.
Halikadhalika viongozi hao wamesema Polisi jamii imewezesha wananchi wakawa na mafunzo mazuri ya kuepuka mambo maovu pia wameomba Jeshi Polisi Mkoa wa Dodoma liendelee na utaratibu huu wa kutembelea kata na tarafa ili kuweza kutoa elimu itakayowapatia mbinu mbalimbali za kuweza kukabiliana na uhalifu na wahalifu.
Wameliomba Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma liendelee na utaratibu wa kuwapatia mafunzo ya udereva vijana wao wanaoendesha pikipiki (bodaboda) ikiwa na pamoja na kuwapatia leseni za udereva ili kuepusha ajali zitokanazo na kutojua sheria za usalama barabarani.
Katika kuhitimisha vikao hivyo na viongozi hao wa tarafa na kata Kamanda MISIME amesema viongozi wa ngazi zote na wananchi wajijengee utamaduni wa kuitisha vikao vya pamoja na kujadili namna ya kubaini viashiria vya uhalifu na migogoro katika maeneo yao.
Pia aliwataka kuzingatia daftari la wakazi ili kuweza kuwajua wakazi wa maeneo yao na kuwatambua wageni na wavamizi ambao wakati mwingine ndiyo chanzo cha migogogo na uhalifu.