Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi DAVID A. MISIME – SACP
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Moto mkubwa umetokea katika eneo la Jamatini Manispaa ya Dodoma na kusababisha hasara ambayo thamani yake bado haijafahamika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi DAVID A. MISIME – SACP, amesema kuwa mnamo tarehe 11/07/2014 majira ya 20:40hrs katika eneo la Jamatini Mkoa wa Dodoma, kulitokea ajali ya moto ulioteketeza vibanda sitini na tatu (63) vya wajasiliamali wadogowadogo ingawa hapakuwa na madhara yoyote kwa binadamu.
Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na hakuna mtu anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hilo.
Aidha Jeahi la Polisi Mkoa wa Dodoma wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kuweza kubaini chanzo cha moto huo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Baadhi ya wajasiriamali wakiokoa mali zao
Kamanda wa Polisi anawapa pole waliounguliwa na vibanda na kupoteza mali zao na kusema kuwa inabidi kila mtu na mamlaka zote kuwa na mipango mizuri wanapojenga nyumba au vibanda vya biashara kuhakikisha wanaacha nafasi ya magari ya huduma kama zima moto kupita kwani katika tukio hili kilichowapa ugumu Jeshi la zimamoto na Polisi kushindwa kuzima moto huo kwa haraka ni kutokana na waliojenga vibanda hivyo hawakuweka njia ya magari ya zima moto kuingia na kuzima moto huo. Tunaamini swala la mipango miji lingezingatiwa vibanda vingi pamoja na mali nyingi kiasi hicho hazingeteketea