Naibu Waziri wa mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba akiwa na mkewe Ramona Makamba wakipokewa na Afisa Ubalozi Mindi Kasiga(wapili toka kushoka) na mwenyekiti wa Vijimambo Baraka Daudi mara tu walipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia. Mhe. Makamba amekuja maalum kama mgeni rasmi kwenye sherehe ya Uhuru wa Tanzania itakayofanyika Jumamosi Desemba 7, 2013 Laurel, Maryland nchini Marekani.
Afisa Ubalozi Mindi Kasiga akimweleza jambo Mhe. January Makamba wakati alipokwenda kumpokea uwanja wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia.
ENDLEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mheshimiwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwenye picha ya pamoja na Makatibu Wakuu na Maafisa wa Ubalozi. Kutoka kushoto ni Bw. Paul Mwafongo (Kaimu Balozi), Bw. George Yambesi (Katibu Mkuu Utumishi), Mhe. January Makamba, Bw. Peter Ilomo (Katibu Mkuu Ikulu), Bw. Suleiman Saleh (Kaimu Mkuu wa Utawala).
Mhe. January Makamba Picha ya pamoja na Ujumbe wa PSPF wakiwemo maafisa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Mhe. January Makamba na mkewe Ramona wakibadilishana mawili matatu na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mindi Kasiga.
Kutoka kushoto ni Afisa Ubalozi Abbas Missana, Afisa Ubalozi Mindi Kasiga, Ramona Makamba na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba.