Wenyeji wa michuano ya kombe la dunia, Brazil, jana walijikuta wakionekana kama timu ya kata mbele ya Wajerumani waliowaangusha mvua ya magoli katika mechi ya nusu fainali.
Mashabiki wa Brazil wakiwa na majonzi makubwa
Kwa ushindi huo wa mabao 7-1 Ujerumani imeingia fainali na sasa inasubiri mshindi kati ya Uholanzi na Argentina ili kufahamu itakayekutana naye.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Brazil walifungwa magoli matano katika kipindi cha kwanza na kuwaacha mashabiki wa Brazil wasiamini macho yao. Hiyo ni aibu kubwa kwa timu ya Brazil kuwahi kufungwa mabao mengi kiasi hicho tangu miaka 80 iliyopita.
“Kila kitu kilikuwa sawa mpaka pale tulipofungwa bao la kwanza,” kocha wa Brazil Luis Scolari alisema. “Kisha, tukajichanganya na baadaye tukaanza kupaniki na kasha kila kitu kikawa vizuri kwa Brazil na kwetu kuwa hovyo.”