Mchangiaji wa mtandao wa Forbes, Rick Smith ameandika makala isemayo 5 Career Mistakes You Will Regret In 10 Years ambayo kutokana na kuwa na maneno muhimu tumeamua kuitafsiri kama ilivyo ili iweze kusomwa na wengine pia.
Wengi wetu tumekuwa tukibadilisha kazi wakati mwingine kwa maamuzi ambayo hayakuona mbali zaidi.Tunajikita katika kumaliza kazi iliyopo mikononi mwetu, kupigania promotion ijayo au kumzidi mwenzako. Lakini kuna vitendo vingi vodogo vinavyoweza kuwa na madhara makubwa kwenye kazi yako. Ukiyaapuuzia unaweza kujikuta kufika katika mwisho ambao hukuutegemea.
Haya ni makosa matano yanayoweza kuwa na madhara kwenye maisha ya kazi yako:
1. Kuwa na network ndani ya kampuni yako pekee.
Watu wengi wanajua kuhusu thamani ya networking. Si ile iliyozoeleka ya kuhudhuria matukio ili tu kugawa business card, lakini ujengaji wa uhusiano halisi. Kuza wigo kwa kutumia mitazamo ya watu wengine. Jifungue kwa kupokea mawazo mapya. Kujenga uhusiano utakaozifanya kazi zako za kila siku kuwa rahisi na zenye kufanikiwa zaidi. Watu wengine huishia kuwa network ndani ya kampuni waliyomo peke yake. Tamaduni zinaweza kuwa tofauti sana, wale waliowahi kufanya kazi kwenye makampuni mbalimbali wanafahamu.
Kujiweka katika mawazo mapya na mitazamo tofauti kunahitaji kutoka nje ya utamaduni na mzunguko wa watu unaoona wanapendeza zaidi kujichanganya nao. Tembea katika zaidi ya bahari moja! Uhusiano mwingi wa kikazi utakaokubadilisha na utakuwa ni ule wa watu walio nje ya kampuni yako – hususan pale mambo yanapokuwa magumu. Inaweza isiwe rahisi lakini kuwekeza katika mahusiano haya ya nje kutalipa.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
2. Kufanya maamuzi kutokana na fedha
Takwimu zinaonesha kuwa hata tukiwa na fedha nyingi kiasi gani bado hujikuta tukitamani kuwa asilimia 20 zaidi. Kubadilishi muelekeo kwa ahadi ya kupata zaidi ni kitu kinachotamanisha. Sote hujikuta tukiona ugumu kupuuzia promotion, kuongezewa mshahara au kubadilisha kampuni ambayo itashibisha akaunti zetu za benki zenye njaa. Lakini siku za mbele katika kazi, unalipwa kwa matokeo uliyoyapata na sio kwa cheo ulichonacho. Chagua mwelekeo utakaokupa uzoefu wenye thamani, utakaozalisha mahusiano yenye tija, na utakaokuruhusu kujifunza zaidi bila kuzingatia kipato. Kuupa kipaumbele uzoefu kuliko kipato kutakupeleka kwenye neema za kweli siku za usoni.
3. Kuepuka Kufeli
Katika maisha ya kazi, mara nyingi utakumbana na njia mbili mbadala za kupitia- moja ikiwa na risk kubwa zaidi. Watendaji wazuri huchanganywa mara nyingi kwa siku zote kuwekwa kwenye kazi zisizoeleweka ambazo wengine walishindwa awali na hakukuwa na dalili za mafanikio. Lakini wenye makampuni huwasimamia hivi waajiriwa bora kwa sababu maalum. Hali ngumu huchochea ukuaji unaokua kwa kasi – sio tu katika kujifunza kuhusu biashara na uongozi, lakini pia katikia kujifahamu wewe mwenyewe. Mafanikio ya muda mrefu hutokana na kupata mkusanyiko wa uzoefu lakini pia kuhamia kwenye kazi ambazo hupanua nguvu na mapenzi yako.
4. Kujenga/Kununua Nyumba????(mmh hii kibongobongo inaweza kutokuwa na ukweli kwakuwa nyumba ni asset muhimu kuwa nayo na hata ukihama unaweza kupangisha au kuiuza)
Ndio, kununua/kujenga nyumba kunaweza kuathiri kazi yako, hasa mwanzoni. Makampuni yanathamini kuhama. Wanataka wafanyakazi wake bora kupata uzoefu mkubwa. Hata katika hatua ya uCEO, bodi hutafuta waombaji wenye uzoefu katika kazi mbalimbali, vitengo mbalimbali ndani ya kampuni. Kununua nyumba kunakufunga katika eneo moja.. Sawa, pale fursa nzuri inapojitokeza, unaweza kuiuza. Lakini makampuni mengi siku hizi hayalipi gharama za kuhama. Na pia jitihada na matumizi yanayohusika katika kuuza nyumba na kuhama yanaumiza kichwa.
5. Kukosa fursa ya kusaidia wengine. Unapofanya kitu kinachotengeneza thamani halisi kwa kampuni ama kwa wengine, utaweza kulipwa kwa hilo siku moja, japo sio mapema. Huu ni ukweli wa maisha katika kazi, japo haufamiki sana. Utafiti unaonesha kuwa wafanyakazi wengi waliofanikiwa kwa mara nne zaidi hujikita katika mafanikio ya watu waliowazunguka kuliko hata kwenye mafanikio yao. Kushinda mechi ndefu katika kazi inahitaji support kubwa kutoka kwa jamaa na wafanyakazi wenza katika kila hatua ya kazi yako. Ukiona fursa ambapo matendo yako yanaweza kuwafaidisha wengine, chukua muda kufanya itokee bila matarajio ya malipo. Hiyo itakufanya upate support ambayo hukuitegemea na ambayo utakuwa ukiihitaji sana.