Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

6 of 1,160 DIAMOND PLATNUMZ ATINGA MDANI YA STUDIO ZA GENN ONLINE RADIO

$
0
0
Mashabiki wa Diamond Platnumz wakipata nae picha ya pamoja na Rais huyo wa Wasafi alipokuwa akiwasili kwenye mji wa Olathe jimbo la Kansas ilipo Radio hiyo ya GENN kwa mahajiano kabla ya show yake inayotarajiwa kufanyika muda si mrefu katika anuani ya 8625 Troost Ave, Kansas City, Missouri.
Mtangazaji wa GENN Radio AJ (mwenye kofia nyeusi wapili toka kulia) akimfanyia mahojiano Diamond Platnumz ndani ya Studio ya Radio hiyo ambayo inapatikana mtandaoni www.gennmedia.com wengine ni Dj Romy Jons Poromota DMK na Dj Bston (kulia) 

ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 
Dj Boston na AJ wakimsikiliza Diamond Platnumz wakati ajibu moja ya maswali waliyomuuliza.
Mashabiki wakiwa ndani ya studio za GENN Radio wakimsikiliza Rais wa Wasafi akijibu maswali aliyokuwa akiulizwa na AJ.
Diamond Platnumz akiendelea kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na AJ huku Dj Romy Jons akifuatilia kwa makini maswali na majibu yaliyokua yakiulizwa AJ na kujibiwa na Diamond Platnumz.
Diamond Platnumz akijibu moja ya maswali kutoka kwa A
Mahojiano yakiendelea Studio za GENN Radio.
Baada ya mahojiano mashabiki nao hawakua nyuma kupata ukodak na prezda wa wasafi ndani ya studi za GENN Radio.
Patrick Joseph wa Wichita akipata picha na Diamond Paltnumz akiwa pamoja na Dj Romy Jones.
Monica Mambo, Neema Mambo na Evelyn Ndungu nao wakipata picha ya pamoja na Diamond Platnumz pamoja na Dj Romy Jons.
Na Mwandishi wetu Kansas.
Diamond Platnumz leo siku ya Jumapili July 6, 2014 alitia timu ndani ya studio za GENN Radio iliyopo mji unaoitwa Olathe uliopo ndani ya Jimbo la Kansas na hii ilikuwa ni baada ya kufanya sound check mida ya saa tisa alasili kwa saa za kati zinazoumia na miji iliyopo magharibi ya kati nchini Marekani  ndani ya Jiji la Kansas jimbo la Missouri uliopo mwendo wa nusu saa toka mji huo wa Olathe ambao wenyewe upo jimbo la Kansas.

Katika mahojiano hayo yaliyoongozwa na
mtangazaji AJ yalizungumzia zaidi Tuzo za BET ambayo Diamond uwepo wake Marekani ni kwa ajili ya tuzo hizo ambaye yeye kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika Mashariki alikuwa nominated na swali la kwanza aliloulizwa na AJ ni anajisikiaje kuwa nominated na BET? Rais wa wasafi kama kawaida yake humtanguliza mwenyezi Mungu mbele kwa kila jambo analofanya alianza kwa kujibu kwa kumshukuru Mungu na kusema kuwa hakutarajia kuwa nominated na alisikia akiwa London nchini Uingereza akirekodi video ya wimbo wake aliposikia habari njema hizo alishangaa kidogo na habari hizo zilizidi kumtia moyo na kumpa ari ya kusonga mbele kwani yeye anaamini maisha ni hatua.

Swali lingine aliloulizwa lilikua kuhusu picha alizopiga Davido wakati anapokea tuzo ya BET, Diamond hakuwemo kwenye picha AJ alitaka kufahamu ni sababu zipi msani huyo wa Bongo flava hakuwemo kwenye hizo picha kwa tafsili nyingine watu wanafikiria ni kwa sababu Diamond hakupendezewa na ushindi wa Davido. Rais wa wasafi Diamond alijibu kwa kuanza kwa kusema si kweli kwamba hakufuarahia ushindi wa Davido sababu ya yeye kutokuwepo kwenye zile picha ni yeye kutokuwepo muda ule pale kwa sababu muda wa kutoa tuzo za wasanii wa Afrika ulibadilishwa usiku wa manane na kuwekwa asubuhi ndio maana hakuwemo kwenye zile picha za Davido.

Swali lingine aliloulizwa Diamond na AJ ni kitu gani alichoona kwenye zile Tuzo za BET ambacho hakupendezwa nacho na  angependa kifanyiwe marekebisho. Diamod ajibu kwa kusema kwa kuwa hii ni BET ni TV ya weusi na yeye anaonelea isingekua vibaya na wao tuzo za wasanii wa Afrika zingerushwa LIVE kwa sababu tunatoka mbali na ndugu zetu wanyumbani walikuwa na shauku ya kutuona LIVE tukipokea tuzo hizo.

Baadae waliruhusu simu za wasikilizaji kumuuliza maswali lakini kila shabiki aliyepiga simu alimpongeza kwa hatua aliyofikia na kumtakia kila la kheri aendelee kupeperusha bendera ya Tanzania. Mwisho Diamond alimalizia kwa kuwaomba mashabiki wake kwamba yeye ni binadamu wanapoona amekosea jambo yeye yupo tayari kuelimishana ni vyema kama kuna lolote lililojema kwa maendeleo tukaelimishana na yeye yupo tayari kulipokea na kulifanyia kazi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>