Gari aina ya Noah likiwa ndani ya mto baada ya kukosea njia na kutumbukia mtoni. Daraja hili liliharibiwa vibaya na Roli tarehe 19/06/2014.Daraja hili linalounganisha Ukonga (Banana)- Tabata Segerea- Kinyerezi na Mbezi
Hii ndio hali halisi ya gari baada ya kutumbukia mtoni hii imetokana na mwendo kasi uliopelekea kuama njia.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Hii ndio speed inayoruhusiwa unapokaribia kwenye daraja hili
Pia katika daraja hili liloharibika kuna kibao kinachoonesha kuwa barabara imefungwa na pia kuna kamba za njano na nyekundu zikionesha kuwa hakuna njia lakini cha kushangaza gari hilo aina ya Noah liliweza kukata kamba hizo na kutumbukia mtoni hii imetokana na mwendo kasi.