Kufuatia tatizo kubwa la maji linaloikabili nchi ya India, wanasayansi wameweza kuitumia vizuri teknolojia na kuanzisha ATM zinazotoa maji kama ATM zinazotoa pesa tulizozizoa.Kufuatia teknolojia hiyo, mwananchi wa kawaida anajiandisha na kupewa ATM kadi maalum ambayo atakuwa anaitumia kupata lita za maji anazotaka kulingana na kiwango cha pesa anacholipa. Mteja anaweza kupata huduma hii masaa 24.
Mteja pia ana nafasi nyingine ya kutumia sarafu kwa kuingiza kwenye ATM hiyo na kuweka kiwango cha lita za maji anazotaka.ATM hizo zinatoa maji safi na salama kwa matumizi ya kunywa kwa kuwa zimefungiwa mtambo maalum wa kusafisha na kuchuja maji.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Hadi sasa mradi huo umekuwa mkubwa na unahudumia watu wengi zaidi na makampuni mengi yamewekeza. Inaelezwa kuwa kuna makampuni ambayo yanatumia teknolojia hiyo pia kusambaza maziwa (ATM ya Maziwa).
Mtanzania hapo vipi….!?