Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

WARSHA YA MUZIKI WA SAMBA REGGE NA SARAKASI KUHITIMISHWA KESHO KWENYE UWANJA WA KASULU, MBURAHATI KWA JONG

$
0
0
 Mkufunzi wa Ngoma za Samba regge, Manni Spaniol akimwelekeza mmoja wa watoto wanaoshiriki warsha ya fit for life iliyoandaliwa na kituo cha Baba watoto cha Mburahati kwa Jongo, Jijini Dar es Salaam.
 Mkufunzi wa ndani, Mwajabu Omari akimwelekeza namna ya kufanya sarakasi mmoja wa watoto wanaoshirika kwenye warsha ya sarakasi na ngomba za samba regge iliyoandaiwa na kituo cha Baba Watoto.

ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 
 Mafunzo ya Sarakasi


 Wanafunzi na wakufunzi wakifanya mazoezi ya kujiandaa na onyesho la muziki wa samba regge litakalofanyika kesho kwenye viwanja vya Kasulu, Mburahati kwa Jongo.
Watoto zaidi ya 80 kutoka kituo cha Baba Watoto kesho wanatarajiwa kupanda katika jukwaa moja kuonyesha ngoma za kibrazili na sarakasi ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha mafunzo ya wiki tatu ya michezo hiyo kupitia mradi wa fit for life yaliyokuwa yakifanyika Mburahati jijini Dar es Salaam.

Warsha hiyo ambayo imewashirikisha watoto walio kwenye mazingira magumu kati ya umri wa miaka 10 hadi 25 imefadhiliwa na umoja wa ulaya (EU) na kusimamiwa na kituo cha Utamaduni cha Ujerumani Goethe-Institut kwa ubia na Ufa-Fabrik ya Ujerumani na Parapanda Theatre.

Meneja mradi wa Fit for life, Habiba Issa amesema kuwa onyesho hilo linafanyika kesho Ijumaa kuanzia saa tisa mchana kwenye kiwanja cha Kasulu Mburahati kwa Jongo, ambapo watoto hao wataonyesha ustadi wa miruko ya sarakasi, trapezi na muziki wa samba regge kutoka nchini Brazil.

Alisema kuwa onyesho hilo litakuwa ndio hitimisha la warsha ya wiki tatu ambayo ililega kuwajengea uwezo watoto na vijana wa kufanya shughuli za sanaa ambazo ni pamoja na ushonaji wa maleba, muziki, ufundi seremala, ujengaji wa majukwaa makubwa na taa na utaalamu wa sauti ya jukwaani.

“Tunategemea vijana hawa watatumia ujuzi huu katika maisha yao ya kila siku maana mwaka jana waijifunza mengi na sasa tumewaongezea uwezo zaidi ili kuwawezesha kujitegemea na kuinua uchumi wao na kuwapa mbinu nyingi za kukabiliana na maisha” alisema Issa.

Akizungumzia maandalizi ya onyesho hilo Msimamizi wa wakufunzi wa ndani katika mafunzo hayo, Mkude Kilosa alisema kuwa vijana wako tayari kwa onyesho hilo na kwamba sasa wako katika hatua za mwisho za maandalizi hayo.

“Mafunzo yanaendelea vizuri na sasa tunajiandaa na onyesho letu la ijumaa ambapo wale waliojiunga nasi mapema wako katika hali nzuri na sasa tunashughulika na hawa wapya ili waweze pia kufanya onyesho siku hiyo” alisema Kilosa

Alisema kuwa mbali na kuwafundisha watoto hao namna ya kucheza sarakasi na muziki wa samba regge pia wanawaandaa kuwa walimu wa sanaa hizo ili waweze kuwafundisha wengine na kukuza vipaji vya watu wengi zaidi nchini
Alisema onyesho hilo linatarajiwa kuwa la kuvutia kutokana ujuzi waliopata watoto hao kutoka kwa wakufunzi wao kutoka Ujerumani, Ufaransa na Kambodia.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles