Mke wa msanii wa vichekesho Mzee Small, Bi Fatuma Saidi amesema marehemu mume wake alikuwa na mpango wa kutoa filamu ya mwisho wakati yupo kitandani.
Akizungumza na mtandao huu leo, Bi Fatuma Saidi amesema kuwa wiki ya mwisho kabla ya Mzee Mzee kufariki alimshauri mke wake afanye filamu wakati yupo kitandani. “Marehemu alikuwa anazungumzia sana suala la kufanya filamu, hata mara ya mwisho siku ya Ijumaa nakumbuka kuna kitu ambacho aliniambia anataka kuniambia, katika wiki nzima alikuwa anasema ninawazo la kutaka nitengeneze mchezo wakati nipo kitandani. Kwa bahati mbaya hakuwahi kufanya hivyo akafariki,” amesema.
Bi Fatuma pia amesema kuwa marehemu Small hakuacha kiporo cha filamu yoyote ambayo ingetarajia kutoa na filamu mwisho kuigiza inaitwa Naondoka Leo na Narudi Leo ambayo ilishatoka.
CHANZO: BONGO 5