Msafara wa Mgeni rasmi ukiwa unaingia katika Viwanja vya Sabasaba
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Wanawake ya Covenant Bi. Sabetha Mwambenja akitoa maelezo machache na Kumkaribisha Mh. Waziri wa Viwanda, Masoko na Biashara Dr. Abdallah Kigoda ili amkaribishe Mgeni Rasmi.
Meza Kuu
Waziri wa Viwanda, Masoko na Biashara Dr. Abdallah Kigoda akielezea mafanikio ya Maonesho ya Sabasaba ikiwa sasa ni ya 38, ambapo yamepanua wigo wa watu wengi zaidi kushiriki kwa kuwapa kipaumbele wafanyabiashara wa ndani ambao wanatengeneza bidhaa zao za hapa hapa ndani ya nchi pamoja na wafanya biashara kutoka nje ya nchi kwa kuongezeka zaidi kwa ushiriki wao katika maonesho ya Sabasaba mwaka huu 2014, Pia kumkaribisha Mgeni Rasmi Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd kuja kuzinduwa Rasmi maonesho hayo.
Mgeni Rasmi Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd akitoa Hotuba yake na kuzindua Rasmi maonesho ya 38 ya Sabasaba
Tuzo mbalimbali kabla ya kutolewa
Baadhi ya wageni mbalimbali walio kuwepo katika uzinduzi rasmi wa maonesho ya 38 ya Sabasaba Jijini Dar es salaam leo
Picha zote na Dar es salaam yetu