Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

BREAKING NEWS: GARI LA MAGEREZA LASHAMBULIWA KWA RISASI NA KUVUNJWA VIOO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
WATU wanaosaidikiwa kuwa majambazi wameshambulia kwa risasi basi la Jeshi la Magereza likiwa na watuhumiwa mbalimbali wakiwamo majambazi sugu na kujeruhi askari wawili.

Habari za uhakika zimeifikia hivi punde kuwa tukio hilo limetokea muda mchache Jumatano Julai 2, 2014 eneo la Mikocheni karibu kabisa na hoteli ya Regency, wakati basi hilo likiwa njiani kutokea mahakama ya Kawe kurudisha watuhumiwa gerezani.

Askari magereza walifanikiwa kuondoka na watuhumiwa hao na haijafahamika mara moja hatima ya majambazi hao lakini askari mmoja amefariki kutokana na hayo mapigano.

Jinsi tukio lilivyotokea

Shuhuda mmoja anasema kuwa, kuna gari ndogo ilikuwa inatokea njia ya Kawe kwenda Shopperz au ilikuwa inaelekea mjini kwa kutumia hii njia ya Mwai Kibaki road. 

Hiyo gari ndogo ilipofika Maeneo ya Million Hairs Salon jirani kabisa na Regency park hotel ikakwama kwenye foleni ndefu sana, nyuma ya hiyo gari ndogo kulikuwa na magari mengine yameunga hiyo foleni.Gari ya magereza ikiwa na wafungwa ilikuwa ni kama ya sita au ya nne nyuma ya hiyo gari ndogo mara ghafla tukasikia puu puuu poo pooo kama risasi 6 au 8 hivi,kumbe ile gari ndogo inavyosemekana ilikuwa imebeba kiasi kikubwa cha pesa na hakukuwa na escort yoyote.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Majambazi wakiwa kwenye pikipiki waliifuata ile gari pale kwenye foleni wakamuamrisha yule jamaa atoe fedha na jamaa akaachia mkwanja. 

Sasa lile gari la magereza kwa vile liko juu sana kama gorofa askari wake wakaiona hiyo inshu live,sasa ile wanajiandaa tu na mabunduki yao' majambazi nayo wakashitukia mchezo na wakaanza wao kuwashambulia kwa risasi wale askari magereza.Askari magereza ile wanajiandaa kujibu mapigo tu majambazi haooooo wakawasha pikipiki na kuondoka kwa speed ya 220.

Kiukweli ilitisha na watu waoga kama mimi nilikimbilia kujificha sehemu,yaani ilikuwa kama Movie.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>