Na MOblog Team
Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam inawashikilia watuhumiwa wawili wa ujambazi wanaohusishwa na mauaji ya mtawa wa kaniasa Katoliki Sista Clezensia Kapuli,
Zaidi ya watuhumiwa hao pia watu wengine sita wanashikiliwa wakihusishwa na matukio mbali mbali ya ujambazi nchini.
Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar esSalaam Kamishna Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari,aliwataja majambazi wanaohusishwa na mauaji ya Sista Kapuli kuwa ni Manase Ogenyeke “mjeshi” (35) mkazi wa Tabata Chang’ombe na Hamis Shaban “Carlos” mkazi wa Magomeni mwembechai
Wengine waliokamatwa kutokana na matukio ya ujambazi ni Beda Mallya miaka (37) mkazi wa Mbezi msakuzi, Michael Mushi (50), Sadick Kisia (32), Elibariki Makumba (30), Nurdini Suleiman (40) pamoja na Mrumi Salehe (38).
Majambazi hao wamekamatwa kutokana na oparesheni kali inayoendelea jijini Dar es Salaam baada ya kifo cha mtawa huyo aliyefariki dunia mnamo Juni 23 mwaka huu.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kova alisema majambazi hao wawili licha ya kuhusishwa na tukio la kifo cha mtawa huyo, pia wanahusika na tukio la uporaji fedha katika benki ya Barcrays tawi la Kinondoni.
“Majambazi hawa walipora mamillioni ya fedha na huyu Ogenyeka ndiye aliyeendesha pikipiki akimbeba jambazi mwenzake ambaye alikuwa na fuko hilo la fedha na kutoroka nazo pia Shabani alikuwa ndiye kiongozi katika tukio hilo,” alisema.
Aidha alisema kuwa jeshi la Polisi bado linawatafuta watuhumiwa wengine wawili katika tukio la mtawa na mmoja kwa jina maarufu Leonard Mollel katika tukio la Barcrays.
Kova alitoa wito kwa wananchi, wafanyabiashara kuachana na mazoea ya kusafirisha fedha kienyeji badala yake watumie njia za kisasa zilizopo sasa nchini.