Mhe. Abdulkarim Shah Mbunge wa Mafya kwa tiketi ya CCM akiongozana na ujumbe wake wa Tanzania Tourist Board (TTB) na Tanzania National Parks (TANAPA) walipowasili Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Washington, DC kwenye chakula cha jioni walipokaribishwa Ubalozini hapo siku ya Alhamisi June 19, 2014. Wengine waliokaribishwa ni Jumuiya ya Watanzania DMV, Kamati ya maandalizi ya sherehe ya Vijimambo, Katibu wa Jumuiya New York alikuwepo lakini chini ya kivuli cha Miss Tanzania USA Pagent chini ya Ma Winny Case. Ujumbe wa TTB na TANAPA ulialianzia New York na wapo nchini Marekani kwa ajili ya kutangaza Utalii wa Tanzania kwa kufanya mazungumuzo na watu mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari kwa ajili ya matangazo na kupata mbinu mbalimbali za kupambana na ujangili wa mali asili na hatimae kuutokomeza kabisa. Mjini New York walipata fulsa ya kufanya mazungumuzo na CNN International na Local na vyombo vingine vya habari yakiwemo magazeti kwa ajili ya kutangaza utalii na mali asili kitu ambacho kinaendelea pia kufanywa na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani chini ya Balozi Mhe. Liberata Mulamula na kufanya nchi ya Marekani kuongoza hivi sasa katika kupeleka watalii wengi nchini Tanzania. Katika picha Mhe. Abdulkarim akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Idd Sandaly.
Mkurugenzi mkuu wa Tanzania National Parks (TANAPA) Bwn. Allan Kijazi akisalimia na mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Ulotu wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani waliokaribishwa chakula cha jioni na Ubalozi wa Tanzania , Washington, DC.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mkurugenzi masoko wa Tanzania Tourist Board (TTB) Bi. Teddy Mapunda akisalimiana na mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Ulotu wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani waliopokaribishwa chakula cha jioni na Ubalozi wa Tanzania , Washington, DC. Nyuma ya Bi. Teddy Mapunda ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Tourist Board Bi. Devota Mdachi akisalimiana na Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Colonel Adolph Mutta.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akifanya utambulisho wa wageni na maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na baadae kuwakaribisha chakula cha jioni.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akijipatia chakula, wengine katika picha ni Mariam Mkama, Edward Taji, Afisa Suleiman Saleh, Mercy Dachi na Rose Mzirai Commodore
kutoka kushoto ni Mrs Esther Zoka Mhe. Abdulkarim Shah, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Bwn Allan Kijazi wakiendelea kujipatia chochote kwenye chakula cha jioni walichakaribishwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Wageni waalikwa wakiwa na mwenyeji wao Balozi Liberata Mulamula kwenye chakula cha jioni.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiongea jambo huku wageni wake wakiendelea na chakula cha jioni.
Mhe. Abdulkarim Shah (watatu toka kushoto) akiwa na mwenyeji wake Mhe. Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na wageni waalikwa kwenye mkaribisho wa chakula cha jioni kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, jijini Washington, DC.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na familia ya Zoka kutoka kushoto ni Andrew Mgendi Zoka, Mrs Esther Mgendi Zoka na kulia ni Mr. Jacky Mgendi Zoka.
Picha ya pamoja.
picha zaidi BOFYA HAPA