Polisi nchini kenya wanasema kuwa watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabaab wamewaua takriban watu 48 kwenye mji wa mpeketoni uliopo karibu na kisiwa cha Lamu.
Watu wanne waliokuwa na silaha waliteka magari mawili na kuyaamrisha kuelekea eneo la Mpeketoni ambapo walianza kuwafyatulia watu risasi kiholela.
Walioshuhudia walisema kuwa kundi moja lilishambulia mikahawa , kituo cha polisi pamoja na kituo cha mafuta kwa saa kadhaa.Miili ilibaki imetapakaa kila mahala huku maeneo mengine yakiteketezwa.
Walioshuhudia shambulizi hilo wanasema makabiliano ya risasi yaliendelea kwa saa kadhaa na kushuhudia majengo yakiteketezwa.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mji wa Mpeketeni uko karibu na kisiwa cha Lamu , eneo linalosifika kama kivutio cha watalii
Kenya imekumbwa na mashambulizi tangu mwaka 2011 ilipopeleka wanajeshi wake nchini Somalia kupambana na wapiganaji wa Al Shabaab
Mashambulizi yanaarifiwa kuanza saa mbili usiku wenyeji walipokuwa wanatazama michuano ya kombe la dunia. Wakazi waliambia BBC kuwa watu waliokuwa wamejihami walivamia gari moja ambalo walilitumia kufanyia mashambulizi katika maeneo tofauti ya Mpeketoni. Wakazi wanasema washambuliaji walikuwa wamejifunika nyuso zao na kisha kutupa maguruneti katika kituo cha polisi kabla ya kuingia na kuiba silaha