Majeruhi akipewa huduma ya kwanza na mmoja wa akina mama aliyekuwa akifanya usafi kando kando ya barabara mapema leo asubuhi,katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha.
Baadhi ya Watu wakitazama ajali ya magari mawili kama yaonekanavyo pichani,iliyotokea mapema leo asubuhi eneo la Moroco-Posta jijini Dar,katika ajali hiyo ambayo chanzo chake hakikufahamika mara moja,mtu mmoja alijeruhiwa na kukimbizwa hospitali kwa huduma ya kwanza,hakuna aliyepoteza maisha.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mama ambaye jina lake halikufahamika mara moja moja aliyekuwa kwenye gari lenye usajili wa namba T679 CKC,akipewa huduma ya kwanza mara baada ya kupoteza fahamu
Moja ya gari ambalo pia lilipata ajali mara baada ya kuacha barabara na kuvamia mtaro kama lionekanavyo pichani.
Moja ya gari ambalo pia lilipata ajali mara baada ya kuacha barabara na kuvamia mtaro kama lionekanavyo pichani,huku abiria wake mmoja akiwa amepoteza fahamu,kama aonekavyo kwa mbali.